Pata taarifa kuu

Viongozi wa nchi za Kirabu na Kiislamu wataka kukomeshwa mara moja kwa vita Gaza

Wito wa kujizuia unaongezeka kutokana na mapigano yanayozidi kuongezeka karibu na hospitali huko Gaza, wakati vita vilivyochochewa na shambulio baya la Hamas nchini Israel mnamo Oktoba 7 vikiingia wiki yake ya sita siku ya Jumamosi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu Hissein Brahim Taha (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Faisal bin Farhan Al Saud (katikati) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Ahmed Aboul Gheit (kulia) Novemba 11, wakati wa mkutano wa kilele kuhus vita huko Gaza.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu Hissein Brahim Taha (kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia Faisal bin Farhan Al Saud (katikati) na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Ahmed Aboul Gheit (kulia) Novemba 11, wakati wa mkutano wa kilele kuhus vita huko Gaza. © AHMED YOSRI / REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wamefutilia mbali siku ya Jumamosi hoja ya Israel ya "kujihami" katika Ukanda wa Gaza na kutaka kusitishwa mara moja kwa operesheni za kijeshi za Israel katika eneo hili. Tamko la mwisho kutoka kwa mkutano wa kilele uliofanyika katika mji mkuu wa Saudia limesema wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na nchi za Kiislamu "wanakataa kutaja vita hivi kama kujihami au kuhalalisha kwa kisingizio chochote kile."

Viongozi hao pia wametoa wito wa kupitishwa kwa "azimio madhubuti na la lazima" kukomesha "uchokozi" wa Israeli katika Ukanda wa Gaza huku wakitangaza kwamba kujiepusha na "kufanya hivyo kunaihimiza Israeli kuendelea na uchokozi wake wa kikatili ambao unaua watu wasio na hatia [...] na huifanya Gaza kuwa magofu."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.