Pata taarifa kuu

Iran yazitaka nchi za Kiislamu kulichukulia jeshi la Israel kama 'kundi la kigaidi'

Akiwa ziarani mjini Riyadh kwa ajili ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu/OIC kuhusu vita huko Gaza, Rais wa Iran Ebrahim Raïssi ametoa wito kwa nchi za Kiislamu kulichukulia jeshi la Israel kama "kundi la kigaidi" kwa sababu ya mashambulizi yake ya anga katika Ukanda wa Gaza. 

Rais wa Irani Ibrahim Raisi amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Riyadh na gavana wa eneo hilo Prince Mohammed bin Abdulrahman bin Aabdulaziz mnamo Novemba 11, 2023.
Rais wa Irani Ibrahim Raisi amepokelewa katika uwanja wa ndege wa Riyadh na gavana wa eneo hilo Prince Mohammed bin Abdulrahman bin Aabdulaziz mnamo Novemba 11, 2023. via REUTERS - WANA NEWS AGENCY
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kwa viongozi wa Kiarabu na Kiislamu waliokusanyika katika mji mkuu wa Saudia, Bw. Raisi pia amezitaka nchi za Kiislamu "kuwapa silaha Wapalestina" ikiwa "mashambulio yataendelea" huko Gaza.

Rais wa Iran Ebrahim Raïssi aliwasili Saudi Arabia siku ya Jumamosi kushiriki katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu na Jumuiya ya nchi za Kiislamu kuhusu vita kati ya Israel na Hamas  katika Ukanda wa Gaza, kwa mujibu wa picha zilizorushwa na televisheni ya serikali ya Saudia ya Al -Ekhbariya.

“Gaza si uwanja wa maneno. Ni lazima tuchukue hatua,” amesema Rais wa Iran Ebrahim Raïssi katika uwanja wa ndege wa Tehran, kabla ya ziara yake kuelekea Riyadh, shirika la habari la REUTERS limeripoti. "Leo hii, umoja wa nchi za Kiislamu ni muhimu sana," ameongeza.

Ni ziara ya kwanza kwa mkuu wa taifa wa Iran nchini Saudi Arabia tangu Tehran na Riyadh kumaliza uhasama wa miaka mingi chini ya makubaliano yaliyofikiwa chini ya mwamvuli wa China mwezi Machi mwaka huu. "Mkutano huo utatuma ujumbe mzito kwa watu wanaochochea vita katika eneo hilo na utapelekea kukomeshwa kwa uhalifu wa kivita nchini Palestina," amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian, ambaye anaongozana na Ebrahim Raïssi, aliyenukuliwa na tovuti ya serikali ya Padolat.

"Marekani inasema haitaki kusambaa kwa vita na imetuma ujumbe kwa Iran na nchi kadhaa. Lakini matamshi haya hayaendani na vitendo vya Marekani,” amesema Ebrahim Raïssi wakati wa maoni ya televisheni katika uwanja wa ndege wa Tehran: "Mashine ya vita huko Gaza iko mikononi mwa Marekani, ambayo inazuia usitishaji vita huko Gaza na kupanua vita. Ulimwengu unahitaji kuona sura halisi ya Marekani."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.