Riyadh yasitisha majadiliano juu ya uwezekano wa kurejesha uhusiano na Israeli
Saudi Arabia imeamua kusitisha majadiliano juu ya uwezekano wa kufufua uhusiano na Israeli, katikati ya vita kati ya Israel na Hamas ya Palestina, chanzo kilicho karibu na serikali ya Saudi Arabia kimeliambia shirika la habari la AFP.
Imechapishwa:
Saudi Arabia "imeamua kusitisha majadiliano juu ya uwezekano wa kufufua uhusiano na Israel na imewajulisha maafisa wa Marekani," amesema, wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, ambaye amezuru Riyadh katika sehemu ya ziara ya kikanda.
Zaidi ya majengo 1,300 yaharibiwa huko Gaza
Zaidi ya majengo 1,300 yameharibiwa kabisa katika Ukanda wa Gaza, Umoja wa Mataifa umesema, baada ya wiki moja ya mashambulizi makali ya wanajeshi wa Israel.
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imesema nyumba 5,540 "ziliharibiwa", wakati karibu zingine 3,750 ziliharibiwa kabisa na haziwezi kukaliwa na watu.
“Tunashuhudia mauaji makubwa na ya kimakusudi ya raia katika eneo hili,” asema Jean-François Corty, naibu mkuu wa shirika la Médecins du Monde kuhusu hali huko Gaza.