Pata taarifa kuu

Maelfu ya Wapalestina wakimbilia kusini mwa Gaza, Israel yakusanya wanajeshi yake

Maelfu ya Wapalestina wanajaribu kukimbia maeneo ya Gaza yanayolengwa na mashambulizi ya angani ya Israeli, baada ya Tel Aviv kuamuru kuhamishwa kwa watu wengi kabla ya shambulio la ardhini.

Wapalestina wakimbia nyumba zao huku kukiwa na mashambulizi ya Israel baada ya Israel kutoa wito kwa zaidi ya raia milioni 1 kaskazini mwa Gaza kuhamia kusini, huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 14, 2023.
Wapalestina wakimbia nyumba zao huku kukiwa na mashambulizi ya Israel baada ya Israel kutoa wito kwa zaidi ya raia milioni 1 kaskazini mwa Gaza kuhamia kusini, huko Khan Younis kusini mwa Ukanda wa Gaza, Oktoba 14, 2023. REUTERS - MOHAMMED SALEM
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, mashambulizi ya Israel huko Gaza yamesababisha "angalau watu 324 kuuawa" katika muda wa saa 24 zilizopita, Wizara ya Afya ya Palestina ya Hamas imesema. Tangu mashambulio ya umwagaji damu yaliyofanywa na Hamas nchini Israel tarehe 7 Oktoba, idadi hiyo imezidi vifo 1,300 kwa upande wa Israel na vifo 2,200 kwa upande wa Palestina. 

"Hatua inayofuata inakuja," Benjamin Netanyahu awaambia askari wake

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametembelea askari wa jeshi la nchi kavu nje ya Ukanda wa Gaza, ofisi yake imesema katika taarifa iliyoambatana na video ambapo amesema, bila kufafanua: "Uko tayari kwa yanayofuata? Hatua hii inakuja."

"Sote tuko tayari," aliandika Waziri Mkuu wa Israel kwenye mtandao wa kijamii wa X, zamani ikiitwa Twitter.

Hezbollah ya Lebanon inasema ililenga ngome za Israel

Hezbollah imetangaza kuwa imelenga ngome za Israel katika eneo la mpaka linalozozaniwa, huku mvutano ukiongezeka kati ya chama cha Kishia na Israel. Mashambulizi haya yanakuja baada ya mwandishi wa habari wa shirika la habari la Reuters kuuawa siku ya Ijumaa na wengine kadhaa, ikiwa ni pamoja na wawili wa shirika la habari la AFP, kujeruhiwa, kwa risasi zilizohusishwa na Israeli na mamlaka ya Lebanon.

Katika taarifa yake, Hebollah inayoiunga mkono Iran imesema imeshambulia maeneo ya Wazayuni katika mashamba ya Lebanon ya Shebaa kwa makombora na roketi. Chama cha hiki cha Kishia kimeongeza kuwa kimelenga ngome hizi "kwa usahihi".

Antony Blinken anaiomba China kutumia "ushawishi" wake katika Mashariki ya Kati

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametoa wito kwa China, mshirika wa Iran, kutumia ushawishi wake kutuliza hali ya Mashariki ya Kati.

Mkuu wa diplomasia ya Marekani, ambaye alikuwa akizuru Saudi Arabia, alifanya mazungumzo ya simu "yenye tija" ya saa moja na mwenzake wa China, Wang Yi, amesema msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller.

Kiongozi wa Hamas wa Palestina anaishutumu Israel kwa "uhalifu wa kivita" huko Gaza

Kiongozi wa Hamas, Ismaïl Haniyeh, ameishutumu Israel kwa kufanya "uhalifu wa kivita" katika Ukanda wa Gaza, eneo lenye watu wengi sana la ardhi ya Palestina, linaloshambuliwa kila mara na jeshi la Israel tangu shambulio la umwagaji damu la Hamas dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba.

"Ukatili wa Israel unajumuisha uhalifu wa kivita na ukiukaji wa wazi wa sheria za kimataifa," ameandika katika barua ya wazi iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, kulingana na taarifa kwenye tovuti ya kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.