Pata taarifa kuu

Israeli inasema imeuua kiongozi wa kundi la Hamas Ali Qadi

Nairobi – Jeshi la Israeli limedai kumuua kiongozi wa kundi la Hamas katika shambulio la angani, ambaye anatuhumiwa kwa aliongoza mashambulio dhidi ya raia kusini mwa Israeli wiki iliyopita.

Makabiliano kati ya jeshi la Israeli na wapiganaji wa Hamas yamekuwa yakiendelea kwa wiki moja sasa
Makabiliano kati ya jeshi la Israeli na wapiganaji wa Hamas yamekuwa yakiendelea kwa wiki moja sasa REUTERS - IBRAHEEM ABU MUSTAFA
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, Israeli imesema Ali Qadi, ameuawa katika shambulio la anga bila ya kueleza shambulio hilo limefanyika wapi na wakati upi.

Hadi tukichapisha taarifa hii, kundi hilo la Palestina halikuwa limezunguzmia madai hayo ya Israeli.

Kwa mujibu wa maofisa wa jeshi la Israeli Qadi, 37, alikuwa kamanda wa kitengo maalum cha wapiganaji wa Hamas waliotekeleza mashambulio dhidi ya raia wake.

Maelfu ya raia wa Gaza wamesemekana kupoteza makazi yao katika mashambulio ya Israeli
Maelfu ya raia wa Gaza wamesemekana kupoteza makazi yao katika mashambulio ya Israeli AFP - MAHMUD HAMS

Taarifa ya Israeli na Palestina ilitihibitisha kuwa Qadi alikuwa miongoni mwa wafungwa walioachiwa huru mwaka wa 2011 kama njia moja ya kubadilishana wafungwa na afisa wa jeshi la Israeli Gilad Shalit, aliyetekwa na Hamas mwaka wa 2006.

Qadi alikamatwa na Israeli mwaka wa 2005 kwa kuhusishwa na utekaji na mauaji ya raia wa Israeli.

Wapiganaji wa Hamas walishambulia Israeli tarehe saba ya mwezi huu na kuwaua zaidi ya raia wa Israeli 1,300 kusini mwa taifa hilo hali iliyopelekea Israeli kujibu.

Tayari raia wameanza kuondoka kaskazini mwa Gaza kwa kuhofia kushambulia katika makombora ya Israeli
Tayari raia wameanza kuondoka kaskazini mwa Gaza kwa kuhofia kushambulia katika makombora ya Israeli AP - Hatem Moussa

Raia zaidi ya 2,215 wameripotiwa kuawaua katika mashambulio ya Israeli katika ukanda wa Gaza.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Vifaa vya WHO vinajumuisha dawa za kutosha kutibu wagonjwa 1,200 waliojeruhiwa na wagonjwa 1,500 wanaosumbuliwa na magonjwa ya moyo, shinikizo la damu, kisukari, na matatizo ya kupumua.

   Pia kuna mifuko ya kiwewe ya kutosha kuwatibu watu 235 waliojeruhiwa, ambayo huwezesha watu waliojeruhiwa kuwa na utulivu na kupata huduma ya haraka ya kuokoa maisha popote inapohitajika.

   WHO ilitoa wito wa kufunguliwa mara moja kwa kivuko cha kibinadamu kupitia Rafah ili kupeleka chakula, mafuta, maji na vitu vingine muhimu vya kujikimu.

   "Waliojeruhiwa vibaya, wagonjwa, na walio hatarini hawawezi kusubiri," alisema.

   Shehena ya kwanza ya misaada ya kibinadamu iliwasili El Arish siku ya Alhamisi kutoka Jordan, vyombo vya habari vinavyohusiana na serikali ya Misri viliripoti.

   Shirika la habari la serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu WAM lilisema UAE ilituma ndege iliyojaa msaada wa matibabu kwa El Arish siku ya Ijumaa.

   Wakati huo huo ndege tatu za Uturuki zilizojaa misaada ya kibinadamu zilitua Jumamosi huko El Arish.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.