Pata taarifa kuu

Saudi Arabia itakuwa mwenyeji wa mikutano ya Jumuiya ya nchi za Kiarabu na Kiislamu wikendi hii

Mikutano ya dharura ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) itafanyika Jumamosi na Jumapili mjini Riyadh, zaidi ya mwezi mmoja baada ya kuanza kwa vita katika Ukanda wa Gaza.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza pamoja na wawakilishi wa mataifa, mashirika ya kimataifa, biashara, benki za maendeleo na mashirika yasiyo ya kiserikali wakati wa mkutano wa kimataifa ambao lengo lake ni kusaidi raia wa Gaza, kwenye ikulu ya rais huko Élysée, Paris, Novemba 9, 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akizungumza pamoja na wawakilishi wa mataifa, mashirika ya kimataifa, biashara, benki za maendeleo na mashirika yasiyo ya kiserikali wakati wa mkutano wa kimataifa ambao lengo lake ni kusaidi raia wa Gaza, kwenye ikulu ya rais huko Élysée, Paris, Novemba 9, 2023. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Wakati hofu ya kuongezeka kwa mapigano katika ukanda huo ikiongezeka, viongozi wa Kiarabu na rais wa Iran watakuwepo kwa mikutano miwili ya kilele inayohusu vita kati ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas kutoka Palestina.

Misri inalaani "ukimya wa kimataifa juu ya ukiukaji wa sheria" unaofanywa na Israeli

Misri imeshutumu leo Alhamisi "ukimya wa kimataifa juu ya ukiukaji wa sheria za kimataifa za kibinadamu unaofanywa na Israel" katika ardhi ya Palestina. Misri imeyasema hayo wakati wa mkutano ambao unalenga kutoa misaada ya kwa raia wa Gaza ulioandaliwa mjini Paris. Kile ambacho serikali ya Israel inafanya kinaenda mbali zaidi ya haki ya kujihami," amesema mkuu wa diplomasia ya Misri Sameh Choukri, akisikitishwa na "kukosekana kwa usawa" katika "jumuiya ya kimataifa."

Hayo yanajiri wakati hapo awali, Israel ilitoa taarifa kuhusu mapigano huko Gaza, ikisema imechukua udhibiti wa "ngome ya Hamas" kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, magharibi mwa Jabalia, baada ya mapigano ya masaa 10.

Hamas sasa pia imetoa taarifa, huku tawi lake la kijeshi, Brigedi za Al-Qassam, likidai kuwa:

  • Imeharibu magari matatu ya Israeli na tingatinga karibu na kambi ya Al-Shati, inayojulikana pia kama kambi ya Pwani.
  • Imeharibu kifaru ya Israel kaskazini mwa Sheikh Radwan katika mji wa Gaza
  • Imeharibu Kifaru ya Israel karibu na eneo la Al-Tawam, kaskazini mwa Gaza City

Wakati huo huo, Vikosi vya Al-Quds - kutoka kundi la Kipalestina la Islamic Jihad - vinadai kushambulia kwa mabomu magari ya Israel katika kambi ya Ansar mjini Gaza.

Pia vinadai kurusha makombora katika mji wa Ashdod nchini Israel, ambapo ving'ora vya mashambulizi ya anga vimesikika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.