Pata taarifa kuu

Gaza: Misri kusaidia kuwahamisha 'karibu wageni 7,000' kupitia kivuko cha Rafah

Misri itasaidia kuwahamisha "karibu watu 7,000" ikiwa ni pamoja na wageni na raia wenye uraia pacha kutoka Ukanda wa Gaza, Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetangaza leo Alhamisi. 

Waandishi wa habari wakinasa habari huku magari ya wagonjwa mahututi kutoka Wizara ya Afya ya Palestina yakipitia lango na kuingia kwenye kivuko cha mpaka cha Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza kabla ya kuvuka kuelekea Misri mnamo Novemba 1, 2023.
Waandishi wa habari wakinasa habari huku magari ya wagonjwa mahututi kutoka Wizara ya Afya ya Palestina yakipitia lango na kuingia kwenye kivuko cha mpaka cha Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza kabla ya kuvuka kuelekea Misri mnamo Novemba 1, 2023. © AFP - MOHAMMED ABED
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano na wanadiplomasia wa kigeni, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ismail Khairat amesema Misri inajiandaa "kurahisisha upokeaji na uhamisho wa raia wa kigeni kutoka Gaza kupitia kivuko cha Rafah" , na kuongeza kuwa kuna na "karibu watu 7,000" na waliwakilisha "zaidi ya mataifa 60". Wizara haielezi ratiba ya mpango wa Misri wa kuwahamisha ria wa kigeni.

Jana, zaidi ya wageni 300 na raia wenye uraia pcha kutoka nchi 15 tofauti waliweza kuondoka Gaza na kuingia Misri. Kwa mfano, zaidi ya Waaustralia 20 walivuka kivuko cha Rafah. Katika ujumbe wa twitter, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia Penny Wong alishiriki picha za raia hawa wa Australia. “Wanasaidiwa na wafanyakazi kutoka Ubalozi mdogo wa Australia nchini Misri. Mipango ya usafiri inafanywa ili waweze kurejea nyumbani, bila gharama zozote,” amebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.