Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Mfungwa wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 23 afariki katika jela la Israel

Mamlaka ya Magereza nchini Israel (IPS) ilitangaza siku ya Jumatatu kifo cha mfungwa wa Kipalestina mwenye umri wa miaka 23 mwenye mfungamano na Fatah, chama cha Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, na kuongeza kuwa "inachunguza" mazingira ya kifo chake.

Gereza la Ayalon karibu na Ramleh, kusini mwa Tel Aviv moja ya magereza ya Israel wanakozuiliwa Wapalestina waliokamatwa.
Gereza la Ayalon karibu na Ramleh, kusini mwa Tel Aviv moja ya magereza ya Israel wanakozuiliwa Wapalestina waliokamatwa. REUTERS/Nir Elias
Matangazo ya kibiashara

Mfungwa huyo, ambaye utambulisho wake haujawekwa wazi, alifariki katika gereza la Meggido kaskazini mwa Israel, IPS imesema katika taarifa yake.

Mpalestina huyo kutoka mji wa Nablus kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na mfuasi wa chama cha Fatah, alikamatwa mwezi Juni 2022 kabla ya kuhukumiwa kifungo kwa "makosa ya usalama", kulingana na chanzo hicho.

"Kama katika tukio lolote la aina hii, mazingira (ya kifo) yatachunguzwa," chanzo hiki kimeongeza.

Mazingira ya kifo hayajulikani

Tume ya Wafungwa, chombo kilicho chini ya Mamlaka ya Palestina, imethibitisha kifo cha mfungwa huyo, ikisema ilikuwa inajaribu kupata maelezo kuhusu mazingira ya kifo chake.

Mnamo Desemba 21, polisi ya Israel ilibaini kuwa karibu walinzi ishirini walihojiwa kabla ya kuachiliwa "chini ya masharti magumu" kama sehemu ya uchunguzi wa kifo cha mfungwa wa Kipalestina kufuatia madai ya ghasia.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Palestina WAFA, Thaer Abu Assab, 38, kutoka mji wa Qalqilya kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, alifariki mwezi Novemba baada ya kupigwa na askari magereza kusini mwa Israel ambako alizuiliwa.

Kuimarishwa kwa masharti ya kizuizini tangu Oktoba 7

Kamati ya Umma Dhidi ya Mateso nchini Israel (PCATI) ilisema kesi hiyo iliibua "tuhuma kubwa kuhusu mabadiliko ya Jeshi la Magereza la Israel kutoka kikosi chenye taaluma kwa kuwalinda wafungwa hadi kuwa jeshi la kulipiza kisasi na kuadhibu."

"Wafungwa sita tayari wamefia gerezani (...) Kesi zote za unyanyasaji na kifo lazima zichunguzwe mara moja," kamati hiyo imeongeza.

Mwanzoni mwa vita kati ya Israeli na Hamas, ambayo ilianza Oktoba 7, wakuu wa magereza wa Israeli walitangaza kuimarisha masharti ya kuwekwa kizuizini kwa wafungwa wa Kipalestina: hakuna tena kuondoka gerezani, hakuna tena kununua chakula kutoka kwenye migahawa wala maduka ya chakula au usambazaji wa umeme gerezani, na kutakuwepo na misako ya kushtukiza ya mara kwa mara.

Kulingana na takwimu za Chama cha Wafungwa wa Kipalestina, chama ambacho kinatetea haki zao, magereza ya Israel yalikuwa na wafungwa 7,800 wa Kipalestina mwanzoni mwa mwezi wa Desemba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.