Pata taarifa kuu

Israeli yaruhusu ukanda wa baharini kwa kupitisha misaada ya kibinadamu kati ya Cyprus na Gaza

Serikali ya Israel imekubali kuundwa kwa ukanda wa baharini kati ya Cyprus na Gaza kwa ajili ya kusafirisha misaada ya kibinadamu. Mizigo hiyo itakuwa ibakaguliwa na Waisraeli kwenye kisiwa cha Ulaya, kabla ya meli kuondoka kuelekea Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Eli Cohen, katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano na mwenzake wa Cyprus Constantinos Kombos, huko Larnaca, Cyprus, Desemba 20, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel Eli Cohen, katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mkutano na mwenzake wa Cyprus Constantinos Kombos, huko Larnaca, Cyprus, Desemba 20, 2023. AP - Petros Karadjias
Matangazo ya kibiashara

Mradi huu wa ukanda utajibu azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la Desemba 22, likitoa wito wa kupanua mifumo ya misaada ya kibinadamu. Mkuu wa diplomasia ya Israel, Eli Cohen, amethibitisha kuwepo kwa ukanda huo wakati wa mahojiano kadhaa Jumapili hii, Desemba 31.

Israel inasema iko tayari kuruhusu kupelekwa kwa misaada ya kibinadamu huko Gaza kwa njia ya bahari. Kama mwanahabari wetu mjini Jerusalem, Michel Paul, anavyoeleza, kanuni hiyo ni rahisi: bidhaa hizo zitakuwa chini ya ukaguzi wa usalama katika bandari ya Cyprus ya Larnaca, kabla ya kusafirishwa hadi ufuo wa bahari kuelekea Palestina, kwa umbali wa kilomita 370.

Bila kupita Misri au Israeli, kwa hivyo, kama ilivyo sasa. Hii itaongeza kwa kiasi kikubwa kiasi cha misaada inayosafirishwa. Tatizo dogo hata hivyo: ukosefu wa miundombinu ya kina cha maji katika pwani ya Gaza.

Kulingana na utafiti uliochapishwa mwaka 2022 na wataalamu wa Marekani na Israel, kina cha maji katika bandari ya Gaza hakizidi mita tano. Kwa hivyo meli zenye kina kifupi sana zitahitajika ili kuweza kuingia bandarini. Bandari ambayo tena kwa mujibu wa utafiti, haina vifaa vya kutosha vya kupakua boti kama korongo kubwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Israel Eli Cohen amezitaja nchi nne za Ulaya kuwa washirika watarajiwa: Ufaransa, Uingereza, Ugiriki na Uholanzi ambazo zote nne zina meli zenye uwezo wa kutia nanga moja kwa moja kwenye pwani ya Palestina.

Iwapo mradi huo utatimia, itakuwa ni mara ya kwanza kulegeza kizuizi cha wanamaji cha Israeli kilichowekwa kwa Gaza tangu mwaka 2007. "Hili linaweza kuanza mara moja," amesema Eli Cohen, ambaye hivi karibuni alitembelea Cyprus kujadili mradi huu na mwenzake.

Jambo hili ni "kiishara zaidi kuliko vitendo", wanabaini waangalizi nchini Misri, nchi ambayo takriban misaada yote ya kibinadamu iliyoletwa Gaza tangu kuanza kwa mzozo hupita, anaripoti mwandishi wetu huko Cairo, Alexandre Buccianti.

Waangalizi nchini Misri hata hivyo wanabaini kwamba ukanda huu wa baharini, mara tu utakapoanzishwa, utafanya uwezekano wa kuja kusaidia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. Mashambulizi ya Israel, kwa hakika, yameitenga kaskazini mwa ardhi ya Palestina, ambayo haipati misaada kutoka Misri. Misaada kwa ajili ya kaskazini mwa Palestina lazima, kwa sasa, itoke Israeli.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.