Pata taarifa kuu

Jeshi la Israel latangaza vifo vya wanajeshi watano huko Gaza tangu Ijumaa

Jeshi la Israel limetangaza siku ya Jumamosi kuwa wanajeshi wake watano wameuawa tangu Ijumaa wakati wakipigana katika Ukanda wa Gaza. 

Jeshi la Israel linaendelea na operesheni zake kuelekea katikati mwa Gaza.
Jeshi la Israel linaendelea na operesheni zake kuelekea katikati mwa Gaza. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wanne waliuawa siku ya Ijumaa kusini mwa Ukanda wa Gaza na wa tano siku ya Jumamosi kaskazini mwa ardhi ya Palestina, jeshi limesema katika taarifa. Vifo hivi vinafikisha 144 idadi ya wanajeshi wa Israel waliouawa tangu kuanza kwa mashambulizi ya ardhini ya jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza tarehe 27 Oktoba.

Hamas yapoteza mawasiliano na kundi ambalo linashikilia mateka watano

Msemaji wa tawi la kijeshi la Hamas Abu Obeida amesema katika taarifa siku ya Jumamosi kwamba kundi lake "limepoteza mawasiliano" na wapiganaji wake waliopewa jukumu la kuwalinda mateka watano wa Israel, wakiwemo wazee watatu walioonyeshwa kwenye video iliyotolewa Desemba 18. "Tunaamini kwamba mateka hawa waliuawa wakati wa shambulio moja la Wazayuni kwenye Ukanda wa Gaza," ametangaza bila maelezo zaidi. Mamlaka ya Israel haikujibu mara moja tangazo la Hamas.

Hamas yadai kuwa zaidi ya watu 200 wauawa katika operesheni za Israeli

Zaidi ya Wapalestina 200 waliuawa katika muda wa saa 24 zilizopita katika mashambulizi ya mara kwa mara ya Israel ya angani na operesheni za ardhini katika Ukanda wa Gaza, Hamas imesema, baada ya azimio la Umoja wa Mataifa kuhusu misaada ya kibinadamu kushindwa kufikia azimio la kutaka kusitishwa kwa mapigano.

Takriban miezi mitatu baada ya kuanza kwa vita kati ya Israel na la Palestina la Hamas, kundi hilo lilitangaza kupatikana kwa miili ya makumi ya Wapalestina waliouawa, ambao baadhi yao limesema "waliuawa" wakati wa operesheni ya ardhini ya Israeli huko Jabaliya, kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.