Pata taarifa kuu

Vita Gaza: Washirika wa Israeli wa Magharibi waongeza shinikizo la kusitishwa kwa mapigano

Serikali ya Israel imekuwa ikikabiliwa na shinikizo kubwa kutoka kwa washirika wake wa nchi za Magharibi tangu makosa ya jeshi la Israel yaliyogharimu maisha ya mateka watatu wa Hamas. 

Jeneza la Alon Lulu Shamriz, mmoja wa mateka watatu wa Israel waliouawa kimakosa na jeshi la Israel wakati wakishikiliwa mateka huko Gaza na kundi la Hamas, wakati wa mazishi yake huko Shefayim, Israel, Desemba 17, 2023.
Jeneza la Alon Lulu Shamriz, mmoja wa mateka watatu wa Israel waliouawa kimakosa na jeshi la Israel wakati wakishikiliwa mateka huko Gaza na kundi la Hamas, wakati wa mazishi yake huko Shefayim, Israel, Desemba 17, 2023. © Violeta Santos Moura / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wito wa kusitisha mapigano unaongezeka. Inabakia kuonekana ikiwa wito huo utasikilizwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.

Wakati huo huo Mkuu wa diplomasia ya Ufaransa Catherine Colonna, akizuru Israel, amesema ana wasiwasi "kwa kiwango cha juu" kwa hali ya Gaza na kutoa wito wa "mapatano mapya ya usitishwaji mapigano wa haraka na wa kudumu". Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Israel, Eli Cohen, amesisitiza msimamo wa serikali ya Israel ambayo kulingana na wito wa kusitisha mapigano ni "zawadi kwa Hamas", iliyoko madarakani katika Ukanda wa Gaza.

Kulingana na vyanzo vya Misri , Israel na Hamas wako tayari kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka, lakini bado wanatofautiana kuhusu utekelezwaji wake.

Hamas inasisitiza kwa upande mmoja kuandaa orodha ya mateka watakaoachiliwa huru na kutaka vikosi vya Israel vijiondoe nyuma ya mstari uliopangwa, vyanzo vimeliambia shirika la habari la REUTERS. Ingawa Israel imekubali kuwa Hamas itatayarisha orodha hiyo, vyanzo vimesema Israel imeomba ratiba na kuona orodha hiyo ili kuweka muda na kuona orodha ili kupanga muda wa kusitisha mapigano. Israeli inakataa kurudi nyuma ya mistari iliyoamuliwa mapema, vyanzo vimeongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.