Pata taarifa kuu

Gaza: Hali ya kibinadamu 'inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku'

Israel inaendelea na mashambulizi yake ya anga kwenye Ukanda wa Gaza mnamo Desemba 15, ikionya kwamba vita hivi vinatarajiwa kudumu "zaidi ya miezi kadhaa."

Katika vifusi vya majengo huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 15, 2023.
Katika vifusi vya majengo huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Desemba 15, 2023. AFP - SAID KHATIB
Matangazo ya kibiashara

Marekani inataka Israel ipunguze kasi ya operesheni zake, huku Joe Biden akimtaka mshirika wake kufanya zaidi kuwalinda vyema raia waliotumbukia katika maafa ya kibinadamu.

Roketi kadhaa zanaswa Jerusalemu

Roketi kadhaa zilinaswa juu ya Jerusalem, muda mfupi baada ya ving'ora vya onyo kupigwa, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wamebaini. Jeshi la Israel limesema ving'ora vilisikika kwa mara ya mwisho mjini Jerusalem tarehe 30 Oktoba. Waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wameona angalau roketi mbili zikinaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel.

Wakati huo huo Baraza la mawaziri la usalama la Israel linasema litaruhusu kupitishwa kwa "muda" msaada wa kibinadamu kwenda Gaza kupitia kituo cha ukaguzi cha Kerem Shalom.

Katika ujumbe wa Twitter, Waziri Mkuu wa Israel amebaini kwamba "kama sehemu ya makubaliano ya kuachiliwa kwa mateka, Israel inajitolea kupeleka chakula na misaada ya kibinadamu kutoka Misri kwa wakazi wa Gaza, kwa lori 200 kwa siku. Kivuko cha Rafah kina uwezo wa kupitisha lori 100 tu kwa siku. Kuanzia sasa na kuendelea, baraza la mawaziri la Israel "limeidhinisha kwa muda upakuaji wa malori upande wa Ukanda wa Gaza, kwenye kivuko cha Kerem Shalom badala ya kurejea Rafah kwa utaratibu".

Katika jumbe nyingine kwenye Twitter, uamuzi wa baraza la mawaziri unaeleza kuwa "msaada wa kibinadamu pekee kutoka Misri ndio utakaohamishiwa Gaza kwa njia hii. Marekani imehakikisha kufadhili uboreshaji wa kivuko cha Rafah haraka iwezekanavyo. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.