Pata taarifa kuu

Saudi Arabia: Viongozi wa Kiarabu na Kiislamu watataka kukomeshwa kwa ghasia Gaza

Viongozi wa nchi za kiarabu na rais wa Iran wanakutana nchini Saudi Arabia siku ya Jumamosi kwa mkutano wa pamoja unaotarajiwa kuangazia udharura wa kukomesha mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza kabla ya mzozo kulikumba eneo nzima.

Ligue arabe Arabie saoudite Riadh
Kikao cha maandalizi ya mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Novemba 9, 2023 mjini Riyadh. AFP - YAZID AL-DUWIHI
Matangazo ya kibiashara

Mikutano ya dharura ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) inafanyika mjini Riyadh wiki tano baada ya kuanza kwa vita vilivyochochewa na mashambulizi ya umwagaji damu ya kundi la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina katika ardhi ya Israel, Oktoba 7.

Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na OIC awali ziliratibiwa kufanya mikutano yao tofauti, lakini Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi imetangaza mapema Jumamosi kwamba mikutano ya kilele ya jumuiya hizo mbili itafanyika kwa pamoja. Uamuzi huu unaangazia hitaji la kufikia "msimamo wa pamoja unaoonyesha mapenzi ya pamoja ya Waarabu na Waislamu kuhusu matukio hatari na ambayo hayajawahi kushuhudiwa katika Gaza na maeneo ya Palestina," Shirika la Habari la Saudi lilisema.

Umoja wa nchi za Kiarabu utajadili "njia ya mbele katika jukwaa la kimataifa kukomesha uchokozi, kuunga mkono Palestina na watu wake, kulaani uvamizi wa Israel na kuiwajibisha kwa uhalifu wake," naibu katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Hossam Zaki,  alisema siku ya Alhamisi.

Islamic Jihad, mshirika wa Hamas huko Gaza, imesema, hata hivyo, kwamba haitarajii "chochote" kutoka kwa mkutano huu. "Hatuweki matumaini yetu katika mikutano kama hii" ambayo haijawahi kutoa matokeo, Mohammad al-Hindi, naibu katibu mkuu wa kundi hilo, alisema Ijumaa katika mkutano na waandishi wa habari huko Beirut.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.