Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron 'ameitaka Israel kukomesha' mashambulizi ya anga yanayoua raia Gaza

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron "ameitaka Israel kukomesha" mashambulizi ya anga yanayowaua raia huko Gaza, katika mahojiano na BBC Ijumaa usiku. “Tunajali maumivu [ya Israeli],” Lakini “pia leo, raia wanakabiliwa na mashambulizi. Watoto hawa, wanawake hawa, wazee hawa wanapigwa mabomu na kuuawa."

Rais Emmanuel Macron wakati wa mkutano kuhusu utoaji misaada ya kibinadamu huko Gaza, Novemba 9, 2023 kwenye Ikulu ya Élysée.
Rais Emmanuel Macron wakati wa mkutano kuhusu utoaji misaada ya kibinadamu huko Gaza, Novemba 9, 2023 kwenye Ikulu ya Élysée. © via Reuters / Pool
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano na BBC siku ya Ijumaa usiku, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron "ameitaka Israel kukomesha" mashambulizi yake yanayoua raia huko Gaza. Rais wa Ufaransa amebaini kwamba "hakuna uhalali" wa mashambulizi yanayoua raia huko Gaza, akitaja "watoto, wanawake na wazee." Alipoulizwa kuhusu uwezekano wa ukiukaji wa sheria za kimataifa na Israel, Emmanuel Macron amesisitiza kwamba yeye sio "jaji", lakini "mkuu wa nchi".

MSF yaonya kuhusu hali katika hospitali ya Al-Shifa

Shirika lisilo la kiserikali la Ufaransa la Madaktari Wasio na Mipaka linaelezea hali mbaya katika hospitali ya Al-Shifa, likibainisha kuwa wahudumu wa afya wanaofanya kazi katika hospitali hiyo "wanahofia maisha yao". Mapema siku ya Ijumaa, hospitali hii ilikumbwa na shambulio lililosababisha vifo vya watu 13, kulingana na Hamas. "Wahudumu wa afya waliogopa, kila mtu akijaribu kuokoa maisha yake na familia yake. Wengine bado wako hospitalini, wengine walikimbia na raia waliokuwa sehemu hiyo,” amesema Maher Sharif, mmoja wa wahudumu wa afya shirika lisilo la kiserikali la MSF huko Al-Shifa. MSF imeomba wafanyakazi, wagonjwa na miundombinu ya matibabu ilindwe.

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Hamas limeripoti vifo kumi na tatu katika shambulio dhidi ya hospitali ya Al-Shifa ambalo limehusishwa Israeli, wakati jeshi la Israeli halikutoa maoni yoyote juu ya operesheni hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.