Pata taarifa kuu

Vita vya Israel na Hamas: Hospitali zakumbwa na mapigano Gaza

Katika siku ya 35 ya vita kati ya Israeli na Hamas, idadi ya watu imezidi watu 11,000 waliouawa huko Gaza, kulingana na Hamas. Siku ya Ijumaa, hospitali kadhaa katika eneo la Palestina zimejikuta katikati ya mapigano na tangu Alhamisi, vifaru vimewekwa karibu na baadhi ya hospitali.

Wagonjwa na watu waliokimbia makazi yao wakipigwa picha katika hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza mnamo Novemba 10, 2023.
Wagonjwa na watu waliokimbia makazi yao wakipigwa picha katika hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza mnamo Novemba 10, 2023. AFP - KHADER AL ZANOUN
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa wizara ya afya ya Hamas, watu kumi na watatu wameuawa katika shambulio la anga dhidi ya hospitali ya Al-Shifa, hospitali kuu ya Gaza. Kwa mujibu wa mkurugenzi wa hospitali hiyo, vifaru vya Israel ndivyo vilivyofyatulia shambulia hospitali hii katikati mwa Gaza siku ya Ijumaa asubuhi. Ua umeharibiwa na shambulio hilo, badala ya moja ya majengo ya hospitali kma ilivyotangazwa hapo awali. Lakini raia wengi wamekimbilia katika hospitali hiyo kwa matumaini ya kuwa salama kuliko nyumbani. Katika video zinazotoka Gaza, kunaonekana damu zikitapakaa chini na miili ya watu ikiwa imelala chini.

Hospitali ya Al-Shifa sio pekee iliyoathiriwa Ijumaa hii. Mohammed Abou Salmiya, mkurugenzi wa hospitali hiyo, amelihakikishia shirika la habari la AFP kwamba "hospitali zote katika mji wa Gaza zimelengwa" na mashambulizi ya jeshi la Israel siku ya Ijumaa. "Hatukutarajia kuona mwaka huu wa 2023 hospitali zikilengwa kwa mashambulizi. Hatuwezi kuhama kwa sababu tuna wagonjwa zaidi ya 60 ambao wako chini ya uangalizi maalum, zaidi ya watoto 50 wakiwa katika mashine za joto inayosaidia watoto wachanga waliozaliwa kabla ya muda wake, wagonjwa zaidi ya 500 wanaotumia dialysis,” anasema.

Kwa mujibu wa shirika la Hilali Nyekundu la Palestina, wanajeshi wa Israel wamefyatua risasi Ijumaa hii kwenye moja ya vituo vyake, hospitali ya al-Quds. Mtu mmoja anaaminika kufariki na wengine kadhaa kujeruhiwa, kwa mujibu wa shirika hilo.

Mapigano pia yanaripotiwa karibu na hospitali ya Al-Awda, huko Jabalia, kaskazini. Na kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza, inayodhibitiwa na Hamas, "vifaru vya Israeli vinazingira hospitali nne magharibi mwa Gaza City." Video zinaonyesha vifaru karibu na majengo haya.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.