Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa: Hali katika Ukingo wa Magharibi ni 'ya kutisha na ya dharura'

Hali katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu ni "ya kutisha na ya dharura" kwa mujibu wa tume ya Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, akisisitiza hasa ghasia za walowezi wa Israel dhidi ya wakazi wa Palestina.

Wapalestina wakitathmini uharibifu uliosababishwa baada ya jeshi la Israel kuvamia kambi ya wakimbizi ya Jenin, Ukingo wa Magharibi, Novemba 3, 2023.
Wapalestina wakitathmini uharibifu uliosababishwa baada ya jeshi la Israel kuvamia kambi ya wakimbizi ya Jenin, Ukingo wa Magharibi, Novemba 3, 2023. © Majdi Mohammed / AP
Matangazo ya kibiashara

Hali katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, ikiwa ni pamoja na Jerusalem Mashariki, "ni ya kutisha na ya dharura kati ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaokua na ya hali tofauti inaoendelea," Elizabeth Throssell, msemaji wa tume ya Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, ametangaza leo Ijumaa wakati wa mkutano kila siku wa Umoja wa Mataifa mjini Geneva.

Kwa upande mwingine, shirika hilo pia limesema "lina wasiwasi mkubwa" juu ya kurejea kwa maelfu ya wafanyikazi wa Kipalestina kutoka Israeli kwenda Ukanda wa Gaza. Maelfu ya wafanyakazi hao, waliokuwa Israel wakati wa mashambulizi ya Hamas mnamo Oktoba 7, "wanarudishwa licha ya hali mbaya" katika Ukanda wa Gaza, ambao umekuwa chini ya mashambulizi makali ya Israel tangu mashambulizi ya kundi la wanamgambo wa Kiislamu wa Hamas, amesisitiza Elizabeth Throssell.

Wakati huo huo Israel imefanya mashambulizi mapya siku ya Ijumaa dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza ambako inaendelea na operesheni zake za ardhini. Israel, ambayo iliahidi "kuangamiza" Hamas, iliyo madarakani katika Ukanda wa Gaza, ilitangaza Alhamisi jioni, baada ya karibu wiki moja ya mapigano ya ardhini, kwamba imeweza kuuzingira mji wa Gaza, ambapo maeneo ya vitongoji yote yamegeuzwa kuwa uwanja wa vita, kwa inajili ya kuharibu "vituo" vya kundi la wanamgambo wa Kiislamu la hamas.

Video zilizotumwa na Hamas zinaonyesha wapiganaji wa kundi la Kiislamu wakitoka kwenye mahandaki kushambulia vifaru vya Israel, ambao maendeleo yao yanafanywa kuwa magumu kutokana na uharibifu huo.

Rais wa Uturuki Erdogan atoa wito wa 'kusitishwa kwa mapigano huko Gaza

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametoa wito siku ya Ijumaa wa "kusitishwa kwa mapigano" haraka iwezekanavyo katika Ukanda wa Gaza na kuhakikisha "kuendeleza" juhudi zake za kumaliza mzozo uliochochewa na shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa la Hamas nchini Israel mapema mwezi Oktoba. "Kipaumbele chetu ni kuanzisha haraka usitishaji mapigano," amesema katika mkutano wa 10 wa kilele wa mataifa ya Turkic huko Astana, mji mkuu wa Kazakhstan.

"Tunafanyia kazi mbinu mpya zitakazohakikisha usalama wa wote, wawe Waislamu, Wakristo au Wayahudi," amehakikisha Bw. Erdogan wakati wa mkutano huu wa kilele unaowaleta pamoja marais wa Azerbaijan, Hungary, Kyrgyzstan, Turkmenistan na Uzbekistan. "Juhudi zetu za kuweka misingi ya mkutano wa kimataifa wa amani zinaendelea," ameongeza. "Ili kuiweka wazi, uhalifu dhidi ya binadamu umefanywa huko Gaza kwa siku 28 hasa," kiongozi wa Uturuki amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.