Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa 'una wasiwasi kwamba uhalifu wa kivita unafanywa'

Umoja wa Mataifa unasema unatiwa wasiwasi na hali inayoendelea katika Ukanda wa Gaza, huku ukibaini kwamba kuna uwezkano kuwa uhalifu wa kivita unafanywa kufuatia mashambulizi ya ulipizaji kisasi ya Israel katika Ukanda huo.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wametoa wito wa "kusitishwa" kwa mapigano katika mzozo kati ya Israel na Hamas kutoka Palestina ili kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa raia huko Gaza, ambayo imezingirwa na ambapo "hakuna aliye katika usalama", unasema Umoja wa Mataifa.
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wametoa wito wa "kusitishwa" kwa mapigano katika mzozo kati ya Israel na Hamas kutoka Palestina ili kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa raia huko Gaza, ambayo imezingirwa na ambapo "hakuna aliye katika usalama", unasema Umoja wa Mataifa. © REUTERS - LISI NIESNER
Matangazo ya kibiashara

“Tuna wasiwasi kwamba uhalifu wa kivita unafanywa. Tuna wasiwasi kuhusu adhabu ya pamoja iliyotolewa kwa wananchi wa Gaza katika kukabiliana na mashambulizi ya kikatili ya Hamas, ambayo pia yanajumuisha uhalifu wa kivita,” amesema Ravina Shamdasani, msemaji wa Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Kibinadamu, wakati wa mkutano wa kila siku wa Umoja wa Mataifa huko Geneva.

Usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi, jeshi la Israeli lilifanya "uvamizi uliolengwa" na vifaru kaskazini mwa Ukanda wa Gaza, ikiwa ni utangulizi wa mashambulizi ya ardhini yaliyotangazwa mara kadhaa na kuthibitishwa Jumatano jioni na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, ambaye aliahidi "kuliangamiza" kundi la Hamas.

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wametoa wito wa "kusitishwa" kwa mapigano katika mzozo kati ya Israel na Hamas kutoka Palestina ili kuwezesha upatikanaji wa misaada ya kibinadamu kwa raia huko Gaza, ambayo imezingirwa na ambapo "hakuna aliye katika usalama", unasema Umoja wa Mataifa.

Kwa jumla, Wapalestina wasiopungua milioni 1.4 wamekimbia makazi yao tangu kuanza kwa vita kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa na mamia ya maelfu ya watu waliokimbia makazi yao wamekusanyika katika mazingira mabaya ya kibinadamu kusini mwa Gaza, karibu na mpaka na Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.