Pata taarifa kuu

Israel yalipua gari la wagonjwa, Mkuu wa WHO 'aghahdabishwa'

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema "ameghadhabishwa  na kitendo hicho". "Tunasema tena: wagonjwa, wahudumu wa afya, vituo vya afya na magari ya wagonjwa lazima vilindwe wakati wote, kila mara,” ameandika kwenye X, zamani ikiitwa Twitter.

Watu wakusanyika karibu na gari la wagonjwa lililooharibiwa katika shambulio la anga la Israeli nje ya hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza mnamo Novemba 3, 2023.
Watu wakusanyika karibu na gari la wagonjwa lililooharibiwa katika shambulio la anga la Israeli nje ya hospitali ya Al-Shifa katika Jiji la Gaza mnamo Novemba 3, 2023. AFP - MOMEN AL-HALABI
Matangazo ya kibiashara

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika Maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu, Lynn Hastings, amesema "amesikitishwa" kwa sababu shambulio hilo limenga "wagonjwa ambao walitarajiwa kuhamishwa ili wawe katika sehemu salama".

 Jeshi la Israel linathibitisha kuwa lililenga gari la wagonjwa, "lililokuwa likitumiwa na Hamas" 

Jeshi la Israel limethibitisha siku ya Ijumaa kuwa lilikuwa likilenga gari la wagonjwa kwenye lango la hospitali kubwa zaidi katika mji wa Gaza, na kuhakikisha kuwa "linatumiwa na kundi la kigaidi la Hamas" ambalo limekuwa kikipigana katika ardhi ndogo ya Palestina tangu Oktoba 7.

Shambulio hili la anga siku ya Ijumaa limesababisha, kulingana na serikali ya Hamas, "dazeni ya vifo na majeruhi". Picha zilizopigwa na shirika la habari la AFP zinaonyesha raia waliojeruhiwa karibu na gari la wagonjwa lililoharibika.

Japan yaahidi msaada wa dola milioni 65 kwa raia wa Gaza

 Akipokewa mjini Ramallah (Ukingo wa Magharibi) na mwenzake wa Palestina Riyad Al-Maliki, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan Yoko Kamikawa amebaini kwamba nchi yake imetoa dola milioni 65 kwa Wapalestina. Pia amekutana na mkuu wa diplomasia ya Israel Eli Cohen na akaomba kusitishwa kwa mapîgano kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.