Pata taarifa kuu

Antony Blinken: Israeli ina 'haki' na 'wajibu' wa 'kujihami'

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amesisitiza leo Ijumaa, wakati wa ziara yake kwa mara nyingine mjini Tel Aviv, kwamba Israel ina na "haki" na "wajibu" wa "kujihami" ili kuhakikisha kwamba shambulio la Oktoba 7 "haliwezi kutokea tena". 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akishuka kwenye ndege yake alipowasili Tel Aviv, Israel, Ijumaa hii, Novemba 3.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akishuka kwenye ndege yake alipowasili Tel Aviv, Israel, Ijumaa hii, Novemba 3. © JONATHAN ERNST / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Tunasalia na imani kuwa Israel sio tu ina haki bali pia wajibu wa kujihami na kufanya kila iwezalo ili kuhakikisha kwamba Oktoba 7 haitatokea tena," Antony Blinken amesema katika akimaanisha shambulio la kundi la wanamgambo wa Hamas kwenye ardhi ya Israel Oktoba 7, baada ya mkutano na Rais wa Israel Isaac Herzog.

FAO yaongeza Palestina kwenye maeneo yanayohitaji msaada wa chakula

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limeiongeza Palestina katika orodha ya nchi na maeneo yanayohitaji msaada wa chakula kutoka nje. "Nchini Palestina, kulingana na mtazamo wa Mahitaji ya Kibinadamu kwa mwaka 2023, watu milioni 1.5 (28% ya raia) walikadiriwa kuwa na uhaba wa chakula na walihitaji msaada wa haraka kati ya mwezi Mei na Julai 2022 (kipindi cha ukusanyaji wa data): Watu milioni 1.2 katika Ukanda wa Gaza na watu 353,000 katika Ukingo wa Magharibi,” linakumbuka shirika hilo.

Wanajeshi wa Israel wakiambataa na vifaru vyao silaha kuelekea mpaka na Ukanda wa Gaza, huku mashambulizi dhidi ya Hamas yakiongezeka, Novemba 3, 2023.
Wanajeshi wa Israel wakiambataa na vifaru vyao silaha kuelekea mpaka na Ukanda wa Gaza, huku mashambulizi dhidi ya Hamas yakiongezeka, Novemba 3, 2023. © AMIR COHEN / Reuters

"Kuongezeka kwa mizozo mwezi Oktoba 2023 kuna uwezekano wa kuongeza hitaji la msaada wa kibinadamu na usaidizi wa dharura, wakati upatikanaji wa maeneo yaliyoathirika unasalia kuwa wa wasiwasi," inaongeza FAO katika ripoti yake ya mtazamo wa mavuno na hali ya chakula inayochapishwa mara tatu kwa mwaka. Shirika hilo linakadiria kuwa jumla ya nchi na maeneo 46 yanahitaji msaada wa chakula kutoka nje.

Waziri Mkuu wa Ireland asema jibu la Israeli ni "kulipiza kisasi"

Mkuu wa serikali ya Ireland, Leo Varadkar, amezungumza na vyombo vya habari vya Ireland wakati wa ziara yake katika mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul. "Nadhani ni muhimu sana kwa kutosahau kamwe jinsi hali ilivyoanza. Awamu hii ya mzozo ilianza kwa shambulio dhidi ya Israel, ambapo raia 1,400 waliuawa,” amesema.

"Kama taifa lolote, Israel ina haki ya kujihami, ina haki ya kuikabili Hamas ili isirudi tena kufanya hivyo," ameongeza. "Lakini ninachokiona kinachotokea kwa sasa sio tu kujihami", "inaonekana zaidi kama kitu cha kulipiza kisasi", amesema Waziri Mkuu wa Ireland.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.