Pata taarifa kuu

Jeshi la Israel latangaza kuwa limekamilisha "kuzingira mji wa Gaza"

Jeshi la Israel limetangaza kwamba limekamilisha "kuzingira mji wa Gaza". "Wanajeshi wetu wamekamilisha kuzingira mji wa Gaza, makao makuu ya kundi la kigaidi la Hamas," msemaji wa jeshi la Israel Daniel Hagari metangaza wakati wa mkutano kuhusu hali katika Ukanda wa Gaza, wiki moja baada ya kuanza kwa operesheni ya ardhini ya Israel katika ardhi ya Palestina.

Gaza baada ya mashambulizi ya Israel.
Gaza baada ya mashambulizi ya Israel. REUTERS - MOHAMMED SALEM
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa tawi la kijeshi la kundi la Hamas kutoka Palestina lilisema kwamba Gaza itakuwa "laana" kwa Israeli, na kuonya kwamba wanajeshi wake wataondoka wakiwa "katika mifuko nyeusi." "Gaza itakuwa laana kwa Israeli," msemaji wa Brigedi ya al-Qassam alisema katika taarifa iliyorekodiwa na vyombo vya habari vya Hamas, akiongeza akiwaambia Waisraeli kwamba wanapaswa kutarajia "kurejeshwa kwa askari (wao) zaidi katika mifuko nyeusi."

Tangu Oktoba 7, Waisraeli 1,400 wameuawa, wakiwemo wanajeshi 333, na jeshi la Israel linaripoti kwamba watu 240 wanashikiliwa mateka na kundi la Hamas. Wapalestina 9,061 wameuawa huko Gaza, wakiwemo zaidi ya watoto 3,500, Wizara ya Afya inayodhibitiwa na Hamas ilmesema saa sita mchana siku ya Alhamisi.

Tunisia yatangaza sheria ya kuharamisha uhusiano wowote na Israel

Ni muswada ambao haujawahi kushuhudiwa ambao umejadiliwa katika Bunge la Tunisia siku ya Alhamisi, anaripoti mwandishi wetu wa mjini Tunis, Lilia Blaise. Muswada huo unaharamisha uhusiano na Israeli, yaani, vitendo vyote vya makusudi vinavyohusisha mawasiliano, propaganda, kuhitimisha mikataba au ushirikiano, moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja na watu wote pamoja na makampuni yanayohusishwa na taasisi ya Kizayuni. Uhusiano unaoaadhibiwa kwa kifungo cha miaka 6 hadi 12 jela.

Lakini utumiaji wa sheria na vipengele vyake vya kiufundi vinaleta tatizo kwa sababu ufafanuzi wa uhalalishaji unajumuisha mambo mengi ya kisheria, kiuchumi, kiutamaduni na hata kugusia suala la watu wenye uraia pacha, kama ilivyokuwa kwa Wayahudi wa Tunisia ambao kwa baadhi yao wana uraia wa Israel.

Kwa hivyo, Alhamisi hii, majadiliano yalilenga zaidi maana ya sheria hiyo katika nchi ambayo uungaji mkono kwa kadhia ya Palestina ni mkubwa. Madhumuni ya muswada huo pia ni kwa kauli moja kati ya wabunge wengi, karibu mia moja kati yao waliwasilisha hoja katikati ya mwezi Oktoba ili kuidhinishwa haraka iwezekanavyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.