Pata taarifa kuu

Israel yadai kunasa kombora kutoka eneo la Bahari Nyekundu

Jeshi la Irael limesema kuwa limenasa kombora kutoka eneo la Bahari Nyekundu na kuharibu baadhi ya ndege sisizo na rubani kutoka Yemen.

Jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi yake Gaza.
Jeshi la Israel linaendelea na mashambulizi yake Gaza. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

"Kombora limerushwa kuelekea eneo la Israeli kutoka eneo la Bahari Nyekundu na limefanikiwa kunaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Arrow, jeshi limesema katika taarifa, muda mfupi baada ya tangazo la Houthis (waasi wa Yemen wanaoungwa mkono na Iran) la kutuma ndege zisizo na rubani kuelekea Israel.

Jeshi la anga la Israel pia limedondosha ndege baada ya kugunduliwa kwa kombora hilo. "Vitisho vyote vya angani vimenaswa nje ya eneo la Israeli," jeshi limeongeza katika taarifa hii kwa vyombo vya habari. "

Kanisa la Orthodox "linalaani" katika taarifa yake "mashambulizi ya anga ya jeshi la Israelidhidi ya Kituo cha Utamaduni cha Orthodox katika kitongoji cha Tal Al-Hawa huko Gaza mapema leo", na kubaini kwamba "shambulio hili linaonyesha dhihirisho la kushangaza la azimio la uharibifu usio na msingi wa Israeli dhidi ya miundombinu ya kiraia na vituo vya huduma za kijamii. Mashahidi huko Gaza wameliambia shirika la habari la AFP kwamba mashambulizi ya anga yameharibu kituo cha kitamaduni cha Orthodox na majengo mengine kadhaa katika eneo hilo. Kwa mujibu wao, jeshi la Israel tangu Jumatatu limetuma maonyo kadhaa kwa wakaazi na watu waliokimbia makazi yao katika kituo hicho ili kuondoka katika eneo hilo.

Kuwaachilia mateka wote bila ubaguzi ni moja ya malengo ya vita vya jeshi la Israeli, anakumbusha mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul. Mwanahabari Barak Ravid amesema kwenye tovuti ya habari ya Axios kwamba mkuu wa Mossad David Barnea alisafiri kwenda Doha wikendi hii ili kujadiliana suluhu la suala la mateka. Matokeo ni chanya, inasemekana, lakini hayajaruhusu mafanikio ya kweli kufikia hatua hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.