Pata taarifa kuu

Ufaransa: Emmanuel Macron kuzuru Israeli Jumanne

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atazuru Tel Aviv Jumanne kukutana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, Ikulu ya Élysée imetangaza hivi punde Jumapili usiku. Ziara ya mkuu wa nchi ya Ufaransa imekuja zaidi ya wiki mbili baada ya mashambulizi mabaya ya Hamas katika ardhi ya Israel, ambayo yalisababisha vifo vya zaidi ya watu 1,400 wakiwemo raia 30 wa Ufaransa. Aidha, watu saba wa Ufaransa bado hawajapatikana.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa nchini Israel tarehe 24 Oktoba 2023.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa nchini Israel tarehe 24 Oktoba 2023. © AFP - BENOIT TESSIER / POOL
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atasafiri hadi Tel Aviv siku ya Jumanne kukutana na Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu, Ikulu ya Élysée imetangaza. Kiongozi wa serikali ya Israel alitangaza muda mfupi kabla kwenye X (zamani ikiitwa Twitter) ziara inayokuja ya rais wa Ufaransa pamoja na waziri mkuu wa Uholanzi Mark Rutte.

Israel yaungwa mkono

Rais wa Marekani Joe Biden, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak tayari wamezuru Israel, kama alivyofanya mkuu wa serikali ya Italia Giorgia Meloni siku ya Jumamosi. Emmanuel Macron kwa upande wake alisema akirejelea kauli yake siku ya Ijumaa kwamba atazuru Mashariki ya Kati ikiwa ataweza "kupata mambo muhimu" kwa ajili ya kanda hiyo kutokana na ziara hii. Kisha akataja, miongoni mwa mambo hayo, "usalama wa Israel", "mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi", kusitishwa kwa mgogoro na kuanza tena "mchakato wa kisiasa" kuelekea suluhisho la serikali mbili, Israeli na Palestina.

Rais wa Ufaransa ameonyesha kuunga mkono bila kushindwa kwa Waisraeli, "haki yao ya kujilinda", lakini pia ametoa wito wa mashambulizi ya Israeli dhidi ya Hamas huko Gaza na kuweza "kutofautisha" Hamas raia wa Palestina.

Joe Biden alijadili vita kati ya Hamas na Israel kwa njia ya simu siku ya Jumapili na Emmanuel Macron, Justin Trudeau wa Canada, Olaf Scholz, Giorgia Meloni na Rishi Sunak.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.