Pata taarifa kuu

Israel-Hamas: Kundi la kwanza la Wafaransa wanaorejeshwa makwao kuwasili Oktoba 12

Ndege ya Air France inawarudisha nyumbani mnamo Oktoba 12 raia waliotambuliwa kama walio hatarini zaidi kati ya raia wa Ufaransa wanaopitia na kuishi Israel. Nchi nyingi za Ulaya zimeanza shughuli za kuwarejesha makwao raia wao walioko Israel kwa sasa.

Ndege maalum ya kwanza ya Air France itawarudisha nyumbani raia wa Ufaransa wanaopitia na kuishi Israel Alhamisi hii, Oktoba 12.
Ndege maalum ya kwanza ya Air France itawarudisha nyumbani raia wa Ufaransa wanaopitia na kuishi Israel Alhamisi hii, Oktoba 12. AFP - ERIC PIERMONT
Matangazo ya kibiashara

Ni kwa ombi la Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa ambapo shirika la ndege la Air France linaandaa zoezi hili la kuwarejesha nyumbani raia hao wa Ufaransa. Hii ni ndege yenye uwezo wa kubeba abiria 380. Itaondoka uwanja wa ndege wa Ben-Gurion huko Tel Aviv pamoja na raia wa Ufaransa saa 4:40 Alaasiri Alhamisi hii, Oktoba 12, na kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Paris Charles de Gaulle, jioni ya Alhamisi.

Ndani ya ndege kuna abiria waliotambuliwa kama walio hatarini zaidi kati ya raia wa Ufaransa wanaopitia na kuishi Israeli. Hawa ni pamoja na watoto ambao hawako pamoja na familia zao, wanawake wajawazito, wazee na watu wenye ulemavu au walio katika hali mbaya ya kiafya.

Kulingana na takwimu za hivi punde zilizotangazwa rasmi, karibu raia 62,000 wa Ufaransa wamesajiliwa kwenye ubalozi mdogo wa Tel Aviv na 25,000 wamesajiliwa na ubalozi mdogo huko Jerusalem. Wafaransa wengi wanaopitia wapo kwa sasa nchini Israel. Zaidi ya maombi 4,000 ya kurejeshwa nyumbani yameripotiwa.

Kwa hivyo ndege ya leo ni ya kwanza. Kuanzia kesho Ijumaa Oktoba 13, safari nyingine za ndege maalum zitaandaliwa kati ya Israel na Ufaransa, Quai d'Orsay ilisema asubuhi ya leo, lakini kwanza kwa watu walio hatarini zaidi.

Wafaransa kumi na wawili waliuawa

Takriban Wafaransa kumi na wawili waliuawa nchini Israel katika shambulio kubwa la kustaajabisha lililoanzishwa na kundi la Hamas wa Palestina na 17 hawajulikani walipo, wakiwemo watoto kadhaa "pengine waliotekwa nyara", kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka Wizara ya Mambo ya Nje.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, Anne-Claire Legendre, alibaini Oktoba 12 kwamba Ufaransa ndiyo nchi pekee ya Ulaya kuwa na taasisi katika Ukanda wa Gaza. Na kwamba watu kadhaa wa Ufaransa, hasa wafanyakazi katika mashirika ya kibinadamu, walikuwepo katika eneo hili. "Tunawasiliana na kila mmoja wao," alisema, akielezea kwamba "sio wote wanataka kuondoka Ukanda wa Gaza."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.