Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Gaza: Zaidi ya mia mbili wauawa na jeshi la Israel katika shambulio dhidi ya hospitali

Watu wasiopunguwa 200 wameuawa Jumanne, Oktoba 17, katika shambulio la anga la jeshi la Israel, IDF, dhidi ya hospitali ya Al Ahli Arab katika mji wa Gaza, mamlaka ya Hamas imetangaza. Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ameshutumu "mauaji" na kutangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.

Watu wakikusanyika karibu na miili ya Wapalestina waliouawa wakati wa mashambulizi ya anga ya Israel kwenye hospitali ya Arab Ahli katikati mwa Gaza, baada ya kusafirishwa hadi hospitali ya Al-Shifa, Oktoba 17, 2023.
Watu wakikusanyika karibu na miili ya Wapalestina waliouawa wakati wa mashambulizi ya anga ya Israel kwenye hospitali ya Arab Ahli katikati mwa Gaza, baada ya kusafirishwa hadi hospitali ya Al-Shifa, Oktoba 17, 2023. AFP - DAWOOD NEMER
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya watu waliouawa katika shambulio la anga la jeshi la Israel imefikia 500, kulingana na BBC ikinukuu msemaji wa wizara ya afya ya Gaza.

Picha zinazotoka katika hospitali ya Al Ahli Arab zinaonyesha matukio ya kutisha - huku watu waliojeruhiwa wakitolewa nje kwa machela gizani.

Miili na magari yaliyoharibiwa yanaonekana yakiwa kwenye barabara iliyojaa vifusi.

Msemaji wa jeshi la Israel anasema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na jeshi linachunguza undani wake.

Ofisi ya vyombo vya habari ya serikali ya Hamas huko Gaza imetaja shambulio hilo dhidi ya hospitali ya Ukanda wa Gaza kuwa ni uhalifu wa kivita.

Katika taarifa, Ofisi ya vyombo vya habari ya serikali ya Hamas imesema: "Hospitali hiyo ilikuwa na makazi ya mamia ya wagonjwa na waliojeruhiwa, na watu walihamishwa kutoka kwa nyumba zao" kutokana na mashambulizi mengine.

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ametangaza siku tatu za maombolezo kufuatia shambulizi la anga katika hospitali ya Al Ahli huko Gaza, vyombo vya habari vya serikali ya Palestina vimeripoti.

Mamia ya watu waliokimbia makazi yao walikuwa wamejihifadhi katika ukumbi kwenye uwanja wa hospitali, kulingana na wenyeji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.