Pata taarifa kuu

Palestina: Nchi za Kiarabu zatoa wito wa kusitishwa kwa oparesheni za kijeshi Gaza

Katibu mkuu wa jumuiya ya nchi za Kiarabu, ametaka kukomeshwa kwa operesheni za kijeshi kwenye ukanda wa Gaza, akisema kuzingirwa na kufungwa kwa eneo hilo ni kunyume na ubinadamu kwa raia wa Palestina.

Jumuiya hiyo inasema lazima Israel isitishe operesheni zake na kuruhusu raia kupokea misaada ya kibinadamu
Jumuiya hiyo inasema lazima Israel isitishe operesheni zake na kuruhusu raia kupokea misaada ya kibinadamu REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao chake na mawaziri wa haki kutoka nchi za Kiarabu, Ahmed Aboul Gheit, amesema ni lazima Israel isitishe operesheni zake na kuruhusu raia kupokea misaada ya kibinadamu.

Israeli imendelea kutekeleza mashambulio katika ukanda wa Gaza
Israeli imendelea kutekeleza mashambulio katika ukanda wa Gaza REUTERS - MOHAMMED FAYQ ABU MOSTAFA

Israel ilitangaza vita dhidi ya kundi la Hamas siku moja baada ya wanamgambo wake kuvuka mpaka wa Gaza wenye ulinzi mkali Oktoba 7, ambapo walitekeleza mauaji ya raia wa Israeli zaidi ya elfu 1.

Ikumbukwe kuwa hili ni shambulio baya zaidi katika historia ya Israel, ambayo nayo ilijubu kwa kuanzisha mashambulio kwenye Ukanda wa Gaza, ambapo yameharibu miundombinu na kuua watu wanaofikia elfu 2 na 700.

Israeli imesema itaendeleza mapambano yake dhidi ya wapiganaji wa kundi la Hamas
Israeli imesema itaendeleza mapambano yake dhidi ya wapiganaji wa kundi la Hamas AP - Ariel Schalit

Haya yanajiri wakati huu Mkuu wa ofisi ya masuala ya kibinadamu Martin Griffiths, akitangaza kuelekea Mashariki ya Kati kujaribu kusaidia upatikanaji wa makubaliano ya kufikisha misaada kwa raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.