Pata taarifa kuu

Brazil kuitisha mkutano wa dharura wa UNSC kuhusu hali Israel na Gaza

Brazil, ambayo kwa sasa inashikilia wadhifa wa urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN), imetangaza Jumamosi Oktoba 7 kwamba itaitisha "mkutano wa dharura wa baraza hilo" kushughulikia hali nchini Israel na Ukanda wa Gaza. 

Wanajeshi wa Israel wametumwa na kuelekea kusini mwa Israel kujibu mashambulizi ya roketi kutoka Ukanda wa Gaza na Hamas, Oktoba 7, 2023.
Wanajeshi wa Israel wametumwa na kuelekea kusini mwa Israel kujibu mashambulizi ya roketi kutoka Ukanda wa Gaza na Hamas, Oktoba 7, 2023. © AMMAR AWAD / Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Serikali ya Brazil inalaani mfululizo wa mashambulizi ya risasi na mashambulizi yaliyofanywa leo nchini Israel kutoka Ukanda wa Gaza," Wizara ya Mambo ya Nje imesema katika taarifa yake, ikitoa wito wa "kujizuia" kwa pande husika ili kuepusha mgogoro.

Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema nchi yake iko kwenye kile ambacho amekitaja kama vita na kundi la wanamgambo wa Palestina Hamas baada ya misururu ya maroketi kurushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel mapema leo Jumamosi.

Jeshi la Israel kwa upande wake limethibitisha kuwa linapambana na wapiganaji wa Gaza walioingia katika himaya kwa njia ya ardhini, baada ya maroketi kurushwa kuelekea Israeli kutoka katika eneo la Palestina.

Maelfu ya askari wa akiba wanatarajiwa kupelekwa huko Gaza, pamoja na kaskazini mwa Israel, karibu na Lebanon na Syria, na Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kimabavu.

Hayo ni baada ya Hamas kutangaza kuwa imeanzisha operesheni 'Al-Aqsa Flood' dhidi ya Israel.

Makumi ya roketi zimerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel Jumamosi asubuhi, Oktoba 7, na kusitisha makubaliano ya kusitisha uhasama yaliyoheshimiwa kwa ujumla tangu kumalizika kwa vita vya siku tano mwezi Mei. Tawi la kijeshi la Hamas limetangaza kwamba limeanzisha operesheni iitwayo "Mafuriko ya Al-Aqsa" dhidi ya Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.