Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Hamas yaanzisha operesheni 'Al-Aqsa Flood' dhidi ya Israel

Makumi ya roketi zmerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel Jumamosi asubuhi, Oktoba 7, na kusitisha makubaliano ya kusitisha uhasama yaliyoheshimiwa kwa ujumla tangu kumalizika kwa vita vya siku tano mwezi Mei. Tawi la kijeshi la Hamas limetangaza kwamba limeanzisha operesheni iitwayo "Mafuriko ya Al-Aqsa" dhidi ya Israel.

Baada ya roketi kurushwa kutoka Ukanda wa Gaza, karibu na nyumba huko Ashkelon, kusini mwa Israeli, Jumamosi, Oktoba 7, 2023.
Baada ya roketi kurushwa kutoka Ukanda wa Gaza, karibu na nyumba huko Ashkelon, kusini mwa Israeli, Jumamosi, Oktoba 7, 2023. AP - Tsafrir Abayov
Matangazo ya kibiashara

"Tumeamua kukomesha uhalifu wowote wa unyakuzi" wa Israel, na "zaidi ya maroketi 5,000" yamerushwa tangu asubuhi ya leo, ametangaza Mohammad Deif, kamanda wa Brigedi za Ezzedine al-Qassam, katika rekodi ya sauti iliyotangazwa na Al-Aqsa TV, televisheni ya Hamas, vuguvugu la wanamgambo wa Kiislamu lililo madarakani huko Gaza. "Ikiwa una silaha, ni wakati wa kuiondoa na kuchukua hatua," Hamas imewaambia Wapalestina.

"Hamas ilifanya makosa makubwa asubuhi ya leo kwa kuanzisha vita dhidi ya Taifa la Israeli," askari wa Israel "wanapigana na adui kila mahali," Waziri wa Ulinzi wa Israeli, Yoav Gallant, ametangaza katika taarifa. Kulingana na idara zake, Bw. Gallant ameidhinisha kurejeshwa kwa askari wa akiba.

Ufyatulianaji wa risasi, kuanzia maeneo kadhaa katika Ukanda wa Gaza, ulianza kabla ya 6:30 asubuhi saa za Mashariki ya Kati na kuendelea karibu dakika arobaini na tano baadaye. Katika Israeli, ving'ora vya onyo vilisikika katika miji kadhaa karibu na Palestina, pia huko Jerusalemu lakini pia ndani zaidi katika eneo hilo, kaskazini na mashariki, kulingana na jeshi.

Roketi zilizorushwa kutoka mji wa Gaza kuelekea Israel, Oktoba 7, 2023.
Roketi zilizorushwa kutoka mji wa Gaza kuelekea Israel, Oktoba 7, 2023. AFP - MAHMUD HAMS

Shambulio ambalo halijawahi kutokea

Roketi imeanguka kwenye mji wa Yavne, kusini mwa Tel Aviv, ambapo mtu mmoja amejeruhiwa kidogo, kulingana na Magen David Adom, sawa na shirika la Msalaba Mwekundu nchini Israel. Mwanamke mwenye umri wa miaka sitini ameuawa "kwa pigo la moja kwa moja", na watu wengine 15 wamejeruhiwa kusini mwa Israeli, linasema shirika la Magen David Adom.

Jeshi la Israel limeripoti kupenya kwa "idadi isiyojulikana ya magaidi" kwenye ardhi ya Israel kutoka Ukanda wa Gaza. "Wakazi katika maeneo jirani ya Ukanda wa Gaza wametakiwa kusalia nyumbani," jeshi limeongeza.Mwezi Mei, Israel ilianzisha mashambulizi dhidi ya Islamic Jihad ya Palestina katika Ukanda wa Gaza, na kusababisha vita vya siku tano kati ya jeshi la Israel, Islamic Jihad na makundi mengine yenye silaha katika eneo hilo, na kugharimu maisha ya Wapalestina 34 na mwanamke mmoja wa Israel.

Katika sehemu ya kuegesha magari huko Ashkelon, kusini mwa Israel, baada ya shambulio la roketi kutoka Gaza, Jumamosi, Oktoba 7, 2023.
Katika sehemu ya kuegesha magari huko Ashkelon, kusini mwa Israel, baada ya shambulio la roketi kutoka Gaza, Jumamosi, Oktoba 7, 2023. AP - Tsafrir Abayov

Zaidi ya roketi elfu moja zimerushwa kutoka Ukanda wa Gaza kuelekea Israel, nyingi zikiwa zimenaswa na mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel. Israel kwa upande wake ilikuwa imeongeza mashambulizi ya anga katika eneo hilo dogo.

Hamas, ambayo ilichukua mamlaka huko Gaza mwaka 2007, ilikuwa imejitenga na mzozo huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.