Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Syria yazika wanajeshi wake waliouawa katika shambulizi la ndege zisizo na rubani Homs

Nchini Syria, mazishi yalianza Ijumaa kwa baadhi ya wahanga 110 wa shambulio la ndege zisizo na rubani wakati wa hafla ya kupandishwa vyeo afisa huko Homs, ambapo Damascus ilijibu kwa mashambulizi makali ya mabomu katika maeneo ya waasi. Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, kwa upande wake, alitoa wito wa "kupunguzwa mara moja" kwa ghasia.

Wanajeshi wakiwa wamebeba majeneza ya wahanga wawili waliouawa katika shambulio dhidi ya chuo cha kijeshi, huko Homs, Syria Oktoba 6, 2023.
Wanajeshi wakiwa wamebeba majeneza ya wahanga wawili waliouawa katika shambulio dhidi ya chuo cha kijeshi, huko Homs, Syria Oktoba 6, 2023. REUTERS - YAMAM AL SHAAR
Matangazo ya kibiashara

Makumi ya ndugu, jamaa na marafiki wa waathiriwa walikusanyika alfajiri ya Ijumaa Oktoba 6 mbele ya hospitali ya kijeshi huko Homs. Magari ya kubebea wagonjwa yalianza kusafirisha hadi kwenye makazi yao ya mwisho mabaki ya maafisa na watu wa familia zao, waliouawa siku moja kabla katika shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye hafla ya kupandishwa vyeo na kusababisha zaidi ya watu 110 wakiwa wameuawa.

"Mwanangu, usiingie kwenye gari, usiondoke, kaa karibu nami," alilia mama mmoja, aliyefadhaika na maumivu, akiwa alivaa nguo nyeusi na maua meupe, kichwa chake kikifunikwa na kitambaa ncheupe.

Askari waliobebelea shada za maua walitangulia majeneza, kwa sauti ya muziki wa kijeshi.

Waziri wa Ulinzi Ali Mahmoud Abbas, ambaye aliondoka kwenye hafla hiyo siku ya Alhamisi muda mfupi kabla ya shambulio la ndege zisizo na rubani, alihudhuria mazishi ya takriban wanajeshi thelathini na raia huko Homs. "Damu ya mashujaa ambao walijitolea maisha yao jana ni muhimu, lakini nchi itawakumbuka zaidi," alisema.

Shambulio la Homs, ambalo lilisababisha "vifo 112 wakiwemo raia 21" na takriban 120 kujeruhiwa, lilihusishwa "makundi ya kigaidi" na jeshi la Syria, ambalo liliahidi "kujibu kwa uthabiti".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.