Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Israel kuingia katika mgogoro wa kikatiba

Mageuzi ya mfumo wa mahakama yanayotarajiwa na serikali ya mrengo wa kulia wa Benjamin Netanyahu yanachochea, pamoja na maandamano ya mara kwa mara, mgogoro mkubwa wa kitaasisi. Mgogoro ambao haujawahi kushuhudiwa unaripotiwa kati ya serikali na wingi wake Bungeni kwa upande mmoja na Mahakama ya Juu kwa upande mwingine. Mahakama ya juu nchini humo inachunguza Jumanne hii kubatilishwa kwa sheria iliyopitishwa mwezi Julai mwaka huu, sheria inayonuiwa kuzuia mamlaka yake.

Maandamano mjini Jerusalem dhidi ya mageuzi ya mfumo wa mahakama Jumatatu Septemba 11 nchini Israel, katika mkesha wa kuchunguzwa kwa rufaa dhidi ya nakala hii na Mahakama ya Juu Jumanne hii.
Maandamano mjini Jerusalem dhidi ya mageuzi ya mfumo wa mahakama Jumatatu Septemba 11 nchini Israel, katika mkesha wa kuchunguzwa kwa rufaa dhidi ya nakala hii na Mahakama ya Juu Jumanne hii. REUTERS - ILAN ROSENBERG
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Jerusalem, Sami Boukhelifa

Israel inazidi kutumbukia katika mzozo hadi kufikia hatua ya kujikuta kwenye hatihati ya mgogoro wa kikatiba. Kama kwingineko, demokrasia ya Israeli inategemea kanuni ya kugawana madaraka: utendaji, utungaji sheria na mfumo wa mahakama; yaani serikali, Bunge na Mahakama ya Juu.

Kwa serikali na Bunge, Mahakama ya Juu ya Israeli ina nguvu zaidi. Mwanzoni mwa mwaka, walizindua mageuzi ya mfumo wa mahakama, ambayo yanalenga kuzuia mamlaka ya mfumo wa mahakama.

Je, marekebisho haya ya mfumo wa mahakaam yana nini?

Kwa mswada huu, serikali inataka kupitia upya mamlaka ya Mahakama ya Juu. Kwa hivyo, inataka kujumuisha kifungu ambacho kitawezesha Bunge, kwa kura nyingi tu, kubatilisha uamuzi wa Mahakama ya Juu.

Marekebisho hayo pia yanapendekeza kuondolewa kwa mawakili kutoka kwa jopo ambalo lina jukumu la kuwateua majaji wa Mahakama ya Juu. Leo hii, linaundwa na kundi la majaji, wabunge na wanasheria kutoka ofisi ya mawakili, chini ya usimamizi wa Waziri wa Sheria.

Serikali pia inataka kuwazuia majaji kutumia hali ya "busara" ya baadhi ya maamuzi ya kisiasa. Nia iliyochochewa na uamuzi wa Januari 18 wa Mahakama uliobatilisha uteuzi wa Arié Dery kama Waziri wa Mambo ya Ndani na Afya kwa sababu ya kupatikana na hatia ya ulaghai wa kodi. Mahakama ya Juu iliona uteuzi huu si "wa busara", hivyo kumshinikiza Waziri Mkuu kumfukuza waziri katika nafasi yake.

Na hatimaye, serikali inataka kupunguza ushawishi wa washauri wa masuala ya kisheria katika wizara mbalimbali kwa sababu mapendekezo yao yanatumiwa na majaji wa Mahakama ya Juu wanapotoa uamuzi kuhusu mwenendo mzuri wa serikali. Kwa hivyo Waziri wa Sheria anataka mapendekezo hayo yachukuliwe waziwazi kama maoni yasiyofungamana na sheria.

Tangu wakati huo, maandamano makubwa yamekuwa yakifanyika kila kukicha kupinga mageuzi haya, kama ilivyokuwa katika maandamano ya jana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.