Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Israeli: Maandamano yanaendelea kushika kasi, licha ya kura ya hatua muhimu ya mageuzi

Siku tano baada ya kura iliyoitikisa Israel, maandamano mengine makubwa yalifanyika Jumamosi usiku huko Tel Aviv na kote nchini kwa Jumamosi ya 30 mfululizo.

Maelfu ya watu waliandamana tena nchini Israeli kupinga mageuzi ya mfumo wa mahakama tarehe 29 Julai 2023.
Maelfu ya watu waliandamana tena nchini Israeli kupinga mageuzi ya mfumo wa mahakama tarehe 29 Julai 2023. AP - Tsafrir Abayov
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa Tel Aviv, Sharon Aronowicz

Maandamano ya watu wenye hasira hayajapungua tangu Bunge la Israeli (Knesset) lilipopitisha, Julai 24, hatua ya kihistoria ya mageuzi ya mfumo wa mahakama yenye utata - kura 64 za ndio, kati ya jumla ya kura 120. Hatua hii sasa inazuia Mahakama ya Juu kubatilisha uamuzi wa serikali kwa madai kuwa "hakuna sababu yoyote" pamoja na kushindwa huku maandamani yanaendelea kushika kasi.

Ujumbe uko wazi: mapambano yanaendelea. Ni makumi ya maelfu, waliopo kwenye nafasi ya demokrasia huko Tel Aviv. Dganit alikuja na mwenzake.

“Tutaendelea kupigana, hatutakata tamaa na hatutawaachia hawa vichaa nchi hii. Niliumia moyoni. Nilikuwa hapa Jumatatu iliyopita na nilipiga mayowe, kitu ambacho sijawahi kufanya katika maandamano hapo awali. "

Mbali na hasira, wengine wanaona kama ushindi kama Itay.

"Kwangu mimi kwa ujumla ni ushindi, wangeweza kupitisha sheria hii miezi sita iliyopita, lakini hawakufanya hivyo kwa sababu ya shinikizo tuliloweka kwao, na onyo la Biden. "

Michal, 38, alikuja na wasichana wake wawili wadogo. Anapigania mustakabali wao na anakataa kuruhusu serikali kuendelea na mageuzi.

“Serikali inajaribu kutunyamazisha lakini ukiangalia huku na kule, haya ni maandamano makubwa zaidi! Watu wanajua kuwa ni muhimu sana kuendelea kuandamana ili kuzuia serikali kushinikiza mahakama. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.