Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-SIASA

Mageuzi ya haki katika Israeli: Benyamin Netanyahu ashambulia askari wa akiba

Waziri Mkuu wa Israel amehutubia taifa hivi pundi siku ya Alhamisi jioni Julai 20 na kutangaza kuwa mageuzi ya mfumo wa mahakama ambayo amekuwa akifanya tangu kurejea kwake madarakani yataimarisha tu demokrasia nchini mwake. Benjamin Netanyahu pia aliwashambulia askari wa akiba ambao waliamua kutojitolea kuhudumu katika jeshi. Harakati ambayo inashika kasi na kuamsha hisia nyingi.

Waziri Mkuu wa Israel Binjamin Netanyahu amewashutumu askari wa akiba wanaopinga mageuzi yake ya mfumo wa sheria wakati wa hotuba yake kupitia televisheni.
Waziri Mkuu wa Israel Binjamin Netanyahu amewashutumu askari wa akiba wanaopinga mageuzi yake ya mfumo wa sheria wakati wa hotuba yake kupitia televisheni. via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Jerusalem, Michel Paul

Maneno ya Benjamin Netanyahu hayashawishi upinzani. Makumi kwa maelfu ya waandamanaji waliingia barabarani na kuzuia barabara kadhaa katika maeneo kadhaa ya nchi Alhamisi hii, Julai 20. Benjamin Netanyahu pia aliwashambulia askari wa akiba ambao waliamua kutojitolea kuhudumu katika jeshi.

Imethibitishwa na video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini Israel na ambayo inasambazwa na mawaziri kadhaa wa mrengo wa kulia wa serikali. Wanajeshi walio katika hali ngumu katika eneo la adui huomba msaada wa ndege. Jibu kutoka kwa marubani ni la kukasirisha: “Je, unaunga mkono mageuzi ya mahakama? wanawauliza.

'Katika demokrasia, jeshi liko chini ya maagizo ya serikali'

Maoni ya Waziri Mkuu yalitolewa siku ya Alhamisi hii, Julai 20 katika taarifa yake kwenye televisheni. Kutotii kunahatarisha usalama wetu, alisema. "Katika demokrasia, jeshi liko chini ya maagizo ya serikali. Sio jeshi linaloamuru nia yake kwa serikali, anasema Benjamin Netanyahu. Ikiwa wahusika katika jeshi wanajaribu kutishia sera ya serikali, ni kinyume na kanuni za demokrasia zote. Na wakifanikiwa kutekeleza tishio lao huo ndio mwisho wa demokrasia, hakika mwisho wa demokrasia! »

Mkuu wa zamani wa Shin Bet anaunga mkono askari wa akiba. Nadav Argaman hata hivyo anazungumzia mapinduzi yaliyoongozwa na serikali. Kwa upande wake Tamir Pardo, mkuu wa zamani wa Mossad, anabaini kwamba Benjamin Netanyahu anapaswa kufikishwa mahakamani ikiwa mageuzi ya mahakama yatapitishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.