Pata taarifa kuu

Ziara ya Ben Gvir kwenye msikiti wa al-Aqsa yazua hasira kwa Hamas na Amman

Kwa mara ya pili katika miezi michache, Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel Itamar Ben Gvir, anayedaiwa kuwa ni Myahudi aliye na msimamo mkali na wa mrengo wa kulia kabisa, amezuru msikiti wa al-Aqsa Jumapili asubuhi, Mei 21. Alifanya ziara hiyo kwa kutaka kujifaharisha, ziara ambayo ilidumu dakika chache na alisindikizwa na maafisa wengi wa polisi.

Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel Itamar Ben Gvir akizuru eneo la Msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem Mei 21, 2023.
Waziri wa Usalama wa Ndani wa Israel Itamar Ben Gvir akizuru eneo la Msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem Mei 21, 2023. © Administration du mont du Temple, via AFP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Jerusalem, Alice Froussard

Ziara hii ni ya "uchochezi" kwa mujibu wa Jordan na Hamas, kwa sababu ni sehemu ya tatu takatifu katika Uislamu, na ambapo ni Waislamu pekee wanaoruhusiwa kinadharia kukusanyika katika eneo hilo takatifu.

Hii si mara ya kwanza kwa waziri huyo kuzuru sehemu hii ambayo ni nyeti sana: Itamar Ben Gvir alikuja kujaribu kama mwanaharakati, kisha kama mbunge, kisha tena kama waziri mwanzoni mwa mwezi Januari sheria hii tete ambayo inasimamia Msikiti.

Kwa nadharia, ni Waislamu pekee wanaoruhusiwa kukusanyika katika eneo hilo: wasio Waislamu wanaweza tu kuingia kwa wakati fulani na hawawezi kuomba, sheria ambayo inafuatwa kidogo na baadhi ya Wayahudi nchini humo. Kwa sababu pia ni mahali patakatifu zaidi katika Uyahudi, ambapo panaitwa Mlima wa Hekalu.

Kwa kuzuru eneo hilo, waziri ana nia ya kudai mamlaka na uhuru wa Israeli juu ya mahali hapa. "Sisi ndio tunaongoza hapa," alisema leo asubuhi. Ziara ya siku chache tu baada ya watu kuandamana kwa bendera katika jiji la kale la Jerusalem, ambalo lina itikadi zaidi kuliko tabia ya kidini.

Hatari ya kuzuka mvutano

Na hata kama ziara hii bado haijaibua milipuko ambayo baadhi ya waangalizi walihofia, tayari imeelezwa kuwa ni uchochezi wa Jordan na Hamas. Jordan, mlinzi wa maeneo takatifu huko Jerusalem, na Hamas huko Gaza tayari wameshutumu ziara hiyo: "Israel itabeba jukumu la uvamizi wa kinyama wa mawaziri wake na makundi yake ya walowezi", linabainisha vuguvugu la Kiislamu lililo madarakani huko Gaza.

Moto unaweza kulipuka katika eneo hilo ndani ya saa chache . Ziara ya Ariel Sharon katika katika msikiti wa al Aqsa alipokuwa kiongozi wa upinzani mwaka 2000 iliibua vita vya pili vya kidini( Intifada). Na mnamo Mei 2021, chokochoko za makundi ya kiitikadi ya Kiyahudi na ukandamizaji uliofuata wa polisi katika eneo hili la kiishara vilisababisha Hamas kufyatua roketi kadhaa na kusababisha vita vya siku 11 huko Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.