Pata taarifa kuu

Israeli yakumbwa na maandamano mapya dhidi ya mipango ya mageuzi ya mahakama

Maelfu ya Waisraeli wameingia barabarani kote nchini katika kile kinachojulikana kuwa maandamano makubwa zaidi katika historia ya Israel. wakati wapinzani wake wanashutumu mageuzi "yasiyo ya kidemokrasia", serikali ya Waziri Mkuu Binjamin Netanyahu, kinyume chake, inatetea "mageuzi muhimu yanayohitajika".

Waandamanaji waandamana dhidi ya mipango ya mageuzi ya mahakama ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, huko Tel Aviv mnamo Julai 18, 2023.
Waandamanaji waandamana dhidi ya mipango ya mageuzi ya mahakama ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, huko Tel Aviv mnamo Julai 18, 2023. © Oded Balilty / AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Jerusalem, Sami Boukhelifa

Maandamano hayo yanapinga mipango ya serikali kupunguza nguvu za Mahakama ya Juu, ambayo wakosoaji wanasema inadhoofisha uhuru wa mahakama na kutishia demokrasia.

Akitetea mipango yake, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alionyesha kuwa mageuzi hayo yatarejesha uwiano kati ya matawi ya serikali.

Suala hilo limesababisha mgawanyiko mkubwa katika jamii ya Israel na kama kiongozi wa upinzani Yair Lapid alivyoeleza, huu ndio "mgogoro mkubwa zaidi" ambao Israeli imekabiliana nao katika historia yake.

Akiwa na umri wa miaka 40, Haïm alihesabu wiki 28 za maandamano dhidi ya mageuzi katika mfumo wa Haki. "Ni wakati wa kuzidisha uhamasishaji, na kuandamana kila siku ikiwa ni lazima", anasema profesa huyu wa chuo kikuu. “Tutafanya hivyo ndani ya mfumo wa sheria na hakutakuwa na vurugu. Mkuu wa polisi alizungumza bungeni akisema kuwa baada ya miezi kadhaa ya maandamano, na huku mamia kwa maelfu ya watu wakiwa mitaani, hakuna hata afisa mmoja wa polisi aliyejeruhiwa. Nguvu yetu ni nguvu ya watu, ya wananchi, ni haki ya kuandamana. Na tunatumia haki hii, kupigania uhuru. "

Raz, pia anafundisha katika Chuo Kikuu cha Kiebrania cha Jerusalem. Kwa profesa huyu wa hisabati, maandamano ni muhimu, lakini sasa ni muhimu wadau wote waungane na kuweka serikali hii "ya kidini na ya msimamo kali", chini ya shinikizo. "Kuna shinikizo la kiuchumi, shinikizo la kijeshi, na pengine shinikizo la kimataifa pia. Vitendo hivi vyote kwa pamoja vinaweza kuleta mabadiliko, nina imani hiyo."

Mara kwa mara tangu mwanzo wa maandamano, wafanyakazi wa teknolojia ya juu, sekta muhimu ya kiuchumi nchini Israeli, wameungana na waandamanaji. Katika jeshi, marubani pia wamekataa kutoa mafunzo kwa kupinga mageuzi hayo.

Hata hivyo serikali imeazimia kutekeleza mageuzi yake katika mfumo wa haki.

Wakosoaji wanasema hii inahatarisha mfumo wa kisiasa, kwani Israel haina katiba na ni bunge pekee linalodhibitiwa na muungano unaotawala.

Katikati ya pambano hili ni Benjamin Netanyahu, ambaye ametawala siasa za nchi hiyo kwa miongo miwili iliyopita.

Licha ya kukabiliwa na kesi kwa madai ya hongo, ulaghai na uvunjaji wa uaminifu, ambayo anakanusha, alichaguliwa tena Novemba 2022 baada ya miezi 18 ya upinzani.

Huu ni muhula wake wa sita kama waziri mkuu na sasa ana wabunge wengi katika Knesset (bunge) akiongoza serikali ya mseto ya vyama vya siasa kali za mrengo wa kulia na kidini.

Tangu serikali iwasilishe mipango ya mageuzi ya mahakama mwezi Januari, maelfu ya watu wameshiriki katika maandamano makubwa ya kila wiki kupinga sheria mpya, ambayo kwa sasa inajadiliwa katika Knesset.

Kura za maoni zinaonyesha mpango wa serikali haupendwi na Waisraeli wengi wangependelea kuafikiana.

Rais Isaac Herzog, ambaye hasa ana jukumu la kiitifaki, amekuwa akishinikiza kuwepo kwa mazungumzo kati ya serikali na upinzani, akionya kuwa nchi hiyo iko ukingoni mwa "kuporomoka kwa katiba na kijamii."

Washirika wengi wa kigeni wa Israel pia wameelezea wasiwasi wao kuhusu sheria hiyo mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.