Pata taarifa kuu

Israel: Mageuzi kwenye idara ya mahakama yazua maandamano makubwa

Hatua ya wabunge nchini Israel kupitisha sheria mpya kuhusu mageuzi kwenye idara ya Mahakama, imezua maandamano makubwa, huku polisi wakikabiliana na waandamanaji wenye hasira.

Maandamano makubwa yashuhudiwa baada ya kupitishwa kwa sheria mpya dhidi ya mahakama
Maandamano makubwa yashuhudiwa baada ya kupitishwa kwa sheria mpya dhidi ya mahakama AP - Ariel Schalit
Matangazo ya kibiashara

Licha ya hasira ya waandamanaji, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu,ametetea uamuzi wa Bunge kupitisha sheria hiyo, akisema ni muhimu ili serikali itekeleze majukumu yake ipasavyo.

Wakati sheria hiyo ikipitishwa, wabunge wa uponzani waliondoka bungeni wakishtumu uamuzi huo wa wabunge walio wengi kutoka upanda wa serikali.

Kabla ya kupitishwa kwa sheria hiyo, mataifa ya nje yakiongozwa na Marekani, yalitoa wito kwa serikali kuachana na mageuzi hayo, kwa kile ilichosema inatishia demokrasia ya nchi hiyo.

Sheria hiyo mpya, inaondoa mamlaka kwa Mahakama ya Juu, kuzuia maamuzi ya serikali, inayoona kuwa haifai.

Waandamanaji wanasema sheria hiyo inatishia demokrasia nchini humo
Waandamanaji wanasema sheria hiyo inatishia demokrasia nchini humo REUTERS - AMIR COHEN

Wapinzani na waandamanaji wanasema, utekelezwaji wa sheria hiyo, inatishia demokrasia ya Israeli na kuigeuza serikali ya Waziri Mkuu Netanyahu kuwa ya kidikteta.

Wapalestina pia wamelaani hatua ya kupitishwa kwa sheria hiyo, ikisema inatoa fursa kwa Israeli kutekeleza sera kandamizi dhidi yao.

Licha ya hasira ya waandamanaji, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu,ametetea uamuzi wa Bunge kupitisha sheria hiyo, akisema ni muhimu ili serikali itekeleze majukumu yake ipasavyo.

Wakati sheria hiyo ikipitishwa, wabunge wa uponzani waliondoka bungeni wakishtumu uamuzi huo wa wabunge walio wengi kutoka upanda wa serikali.

Sheria hiyo kwa muda sasa imekuwa ikizua maandamano makubwa nchini humo
Sheria hiyo kwa muda sasa imekuwa ikizua maandamano makubwa nchini humo AP - Ohad Zwigenberg

Kabla ya kupitishwa kwa sheria hiyo, mataifa ya nje yakiongozwa na Marekani, yalitoa wito kwa serikali kuachana na mageuzi hayo, kwa kile ilichosema inatishia demokrasia ya nchi hiyo.

Sheria hiyo mpya, inaondoa mamlaka kwa Mahakama ya Juu, kuzuia maamuzi ya serikali, inayoona kuwa haifai.

Wapinzani na waandamanaji wanasema, utekelezwaji wa sheria hiyo, inatishia demokrasia ya Israeli na kuigeuza serikali ya Waziri Mkuu Netanyahu kuwa ya kidikteta.

Wapalestina pia wamelaani hatua ya kupitishwa kwa sheria hiyo, ikisema inatoa fursa kwa Israeli kutekeleza sera kandamizi dhidi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.