Pata taarifa kuu
HAKI-MAANDAMANO

Israel: uhamasishaji dhidi ya mageuzi ya mahakama na serikali ya Netanyahu waendelea

Harakati dhidi ya mageuzi ya mahakama zinaendelea kushika nchini Israel. Kama kila Jumamosi jioni na kwa wiki ya 34 mfululizo, wapinzani wa mradi huo walikusanyika katika miji mikubwa lakini pia kwenye madaraja na njia panda Jumamosi Agosti 26. Mmoja wao hata alisimama mbele ya makazi ya rais wa Israel huko Jerusalem. Maandamano hayo pia yanahusu masuala mengine, ikiwa ni pamoja na kukaliwa kwa mabavu maeneo ya Wapalestina.

Maelfu ya waandamanaji katika mitaa ya Tel Aviv, Agosti 26, 2023.
Maelfu ya waandamanaji katika mitaa ya Tel Aviv, Agosti 26, 2023. AFP - JACK GUEZ
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul

Makumi ya maelfu ya waandamanaji walikusanyika kote nchini kuendelea kupinga mageuzi ya mfumo wa mahakama. Lakini wiki hii pia walikuwa wakipinga udhaifu wa serikali katika kukabiliana na ghasia ndani ya jumuiya ya Waarabu, lakini pia dhidi ya matamshi ya waziri wa siasa kali za mrengo wa kulia Itamar Ben Gvir kuhusu usalama wa Wayahudi ambao walishinda uhuru wa kutembea. kwa Waarabu.

'Hawajali chochote'

Tomer alikuja hasa pamoja na kundi la marafiki kupinga maneno haya: “Hata kabla hajatoa matamshi yake ya kutisha na ya kibaguzi, ilifikiriwa kwamba alikuwa akichochea ugaidi. Kiwango ni cha chini sana hata wanatambua kuwa kuna ubaguzi wa kutisha dhidi ya Wapalestina. Na hawajali! "

Waandamanaji hao pia walikuwa wakipinga uungaji mkono wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa waziri wake. Kwa mujibu wa Mikha, mwanaharakati anayeunga mkono Palestina, mwelekeo uko wazi: “Hii ni dhibitisho kwamba demokrasia na uvamizi haviendani pamoja. Mrengo wa kulia daima huimarika wakati kunaripotiwa uvamizi. Hakuna cha kufanya. Na tunaweza kuona sasa kwamba ubaguzi wa rangi umeingia serikalini. Sasa imekuwa halali. Ni jambo jipya hili. Na yote ni kwa sababu ya uvamizi. "

Maandamano zaidi yanapangwa katika siku zijazo, baadhi ya maandamno hayo yanatarajiwa kufanyika mbele ya nyumba za mawaziri katika makazi ya watu wengi katika Ukingo wa Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.