Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Iran: Watu wanne wauawa katika shambulizi kwenye madhabahu takatifu ya Washia

Watu wanne wameuawa katika shambulio la Jumapili kwenye madhabahu takatifu ya Shah-Cheragh ya Washia nchini Iran, kulingana na vyombo vya habari vya serikali.

Picha kutoka ndani ya kwenye madhabahu takatifu ya Shah-Cheragh  baada ya shambulio lililodaiwa na IS ambalo liliua watu wasiopungua 15 mnamo Oktoba 26, 2022.
Picha kutoka ndani ya kwenye madhabahu takatifu ya Shah-Cheragh baada ya shambulio lililodaiwa na IS ambalo liliua watu wasiopungua 15 mnamo Oktoba 26, 2022. AP - Mohammadreza Dehdari
Matangazo ya kibiashara

"Takriban watu wanne waliuawa kufuatia shambulio la kigaidi lililotekelezwa na watu wawili wenye silaha dhidi ya madhabahu takatifu ya Shah-Cheragh" huko Shiraz, mji ulio kusini mwa Tehran, kulingana na shirika rasmi la habari la Irna. Mmoja wa washambuliaji alikamatwa huku mwingine akiwa bado hajakamatwa, kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim.

Wanaume wawili wahusika katika shambulio hili

Mmoja wa washambuliaji amekamatwa, huku mwingine akiwa bado hajakamatwa, kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim. Shah-Cheragh, eneo muhimu sana la mahujaji wa Kishia nchini Iran, lililengwa na shambulio lililosababisha vifo vya watu 13 mnamo Oktoba 26, 2022.

Wanaume wawili waliohusika katika shambulio hili lililodaiwa na kundi la wanajihadi la Islamic State (IS) walinyongwa hadharani huko Shiraz mnamo Julai 8. Watu hao wawili walipatikana na hatia ya "ufisadi katika ardhi ya Iran, uasi wa kutumia silaha na kuhatarisha usalama wa taifa", pamoja na "njama dhidi ya usalama wa nchi". Pia walishtakiwa kwa kuwa uhusiano na kundi la Islamic State na "njama dhidi ya usalama wa nchi".

ISIS ilidai kuhusika na shambulio lake la kwanza nchini Iran mnamo 2017

Mizan Online, shirika rasmi la Mamlaka ya Mahakama, liliwataja watu wawili walionyongwa kuwa ni Mohammad Ramez Rashidi na Naeem Hashem Qatali, bila kufichua uraia wao. Mnamo mwezi Novemba, mamlaka ilisema "magaidi 26 wa Takfiri" kutoka Afghanistan, Azerbaijan na Tajikistan walikamatwa kuhusiana na shambulio hilo.

Iran, nchi yenye Washia wengi, neno takfiri kwa ujumla hurejelea wanajihadi au wafuasi wa Kiislamu wenye itikadi kali wa Kisunni. IS ilidai shambulio la kwanza nchini Iran mnamo 2017, wakati watu wenye silaha na washambuliaji wa kujitoa mhanga waliposhambulia jengo la bunge huko Tehran na kaburi la Ayatollah Ruhollah Khomeini, mwanzilishi wa Jamhuri ya Kiislamu, na kuua watu 17 na kujeruhi makumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.