Pata taarifa kuu

Iran yatangaza makubaliano ya kubadilishana wafungwa na Marekani

Iran imethibitisha kuachiliwa kwa wafungwa wa Kimarekani waliokuwa kwenye jela ya Evin huko Tehran kama sehemu ya makubaliano ya kubadilishana wafungwa na Marekani, shirika la habari la serikali la IRNA limeripoti. "Chini ya makubaliano haya, wafungwa watano wa Iran nchini Marekani na wafungwa watano wa Marekani nchini Iran watakabidhiwa mamlaka husika katika nchi hizi", limetangaza shirika la Irna, likinukuu chanzo cha serikali.

Wafungwa sita wa Marekani wameachiliwa huru kufuatia makubaliano kati ya Iran na Marekani.
Wafungwa sita wa Marekani wameachiliwa huru kufuatia makubaliano kati ya Iran na Marekani. © DON EMMERT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wafungwa wanne, Wairan wenye asili ya Marekani Siamak Namazi, Emad Sharqi, Morad Tahbaz, pamoja na mfungwa mwingine ambaye jina lake halijatajwa, waliondoka katika gereza la Evin siku ya Alhamisi ili kuhamishwa kwenye kifungo cha nyumbani, familia ya mmoja wao ilitangaza mapema Alhamisi. Kesi ya mfungwa wa tano, mwanamke wa Kimarekani , ni sehemu ya mazungumzo. Tayari amejiunga na kifungo cha nyumbani wiki chache zilizopita.

Shirika la Irna limethibitisha habari hii, likinuku  ujumbe wa Iran kwa Umoja wa Mataifa. Wamarekani wote wanaozuiliwa wana asili ya Iran. Iran haitambui uraia pacha na haikuwa na uhusiano wa kidiplomasia na Marekani tangu Mapinduzi ya Kiislamu ya 1979.

Majadiliano kuhusu kutolewa kwa euro bilioni sita 

Hatua iliyofikiwa kuelekea kuachiliwa kwa wafungwa hao inakuja baada ya mazungumzo mengi ya siri na magumu kati ya Washington na Tehran. Iran ilithibitisha mwezi Juni kuwa inafanya mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani kupitia Ufalme wa Oman, mpatanishi wa jadi kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na mazungumzo hayo, yalilenga katika kuachia dola bilioni sita za fedha za Iran zilizokuwa zinazuiliwa nchini Korea Kusini kwa akaunti maalum nchini Qatar. Nchi hiyo ilikuwa imezuia fedha hizi, kutokana na mauzo ya hidrokaboni na Iran, kufuatia vikwazo vya Marekani. Iran inaweza kutumia fedha hizi kwa ununuzi wa misaada ya kibinadamu, kama vile chakula na dawa.

Alipoulizwa kuhusu suala hilii, mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken, hata hivyo, alifafanua siku ya Alhamisi jioni kwamba "Iran haitaondolewa vikwazo". "Fedha za Iran zinapaswa kutumika na kuhamishiwa kwenye akaunti zilizowekewa vikwazo ili zitumike tu kwa madhumuni ya kibinadamu," alisema.

Ikiwa yote yatafanyika kama ilivyopangwa, wafungwa wanaweza kuondoka Iran mwezi Septemba, kulingana na chanzo kinachofahamu suala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.