Pata taarifa kuu

Nyuklia ya Iran: Tehran yataka makubaliano mapya kutoka kwa Marekani

Iran imetuma majibu yake kuhusu suala la nyuklia kwa Josep Borell, mkuu wa diplomasia ya Ulaya, huku ikiweka masharti yake. Hii ni wakati Umoja wa Ulaya (EU) ulikuwa umethibitisha kuwa nakala iliyowasilishwa ilikuwa ya "mwisho" na kwamba ilipaswa kuchukuliwa au kuachwa.

Bendera ya Iran ikipepea mjini Vienna, Austria, ambako mazungumzo ya nyuklia ya Iran yalifanyika.
Bendera ya Iran ikipepea mjini Vienna, Austria, ambako mazungumzo ya nyuklia ya Iran yalifanyika. © AP Photo/Florian Schroetter, FILE
Matangazo ya kibiashara

Jibu la Tehran, lililotumwa kabla ya saa sita usiku, linadai makubaliano zaidi kutoka kwa Marekani. "Iran imeelezea wasiwasi wake juu ya masuala kadhaa ambayo hayajakamilika. Haya si masuala ambayo nchi za magharibi hazikuweza kuyatatua. Tuko karibu kufikia makubaliano, lakini kabla matatizo haya hayajatatuliwa, kazi haijakamilika, "amesema Seyed Mohammad Marandi, mshauri wa timu ya mazungumzo ya Iran, ameripoti mwandishi wetu wa Tehran, Siavosh Ghazi.

Kufikia jana, Mkuu wa Diplomasia ya Iran Hossein Amir Abdollahian alikuwa amebainisha kwamba Wamarekani wameonyesha kubadilika kwa kauli katika masuala mawili kati ya matatu yaliyosalia, lakini kwamba Iran ilitaka kupewa dhamana kwamba Washington haitajiondoka tena - kama ilivyofanya mezi Mei 2018 - kwenye makubaliano ya nyuklia ya Julai 2015. Hii ina maana kwamba mamo bado hayajakamilika. Hasa tangu msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Ned Price alijibu kwa kusema kwamba Tehran inapaswa kuacha madai yake "ya kupita kiasi".

Pamoja na vita vya Ukraine, mzozo wa nishati unapokaribia majira ya baridi na maendeleo makubwa katika mpango wake wa nyuklia, Tehran inabaini kwamba iko katika nafasi ya nguvu na inataka kupata makubaliano ya juu zaidi kutoka kwa Marekani na nchi za Ulaya kabla ya makubaliano yoyote. Kwa upande wake, Umoja wa Ulaya "unajaili" majibu ya Iran kwa "nakala ya mwisho" iliyotolewa na EU kuokoa makubaliano ya 2015 juu ya faili ya nyuklia ya Iran, "kwa kushauriana na washirika wake", alitangaza Jumanne msemaji wa Tume ya Umoja wa Ulaya.

Baada ya miezi kadhaa ya mkwamo, majadiliano yalianza tena mnamo Agosti 4 katika mji mkuu wa Austria kwa jaribio jingine la kuokoa mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran, chini ya uangalizi wa Umoja wa Ulaya, makubaliano ya kimataifa yalihitimishwa mnamo mwaka 2015 kati ya Iran uapande mmoja na Marekani, Uingereza, China, Ufaransa, Ujerumani na Urusi, upande mwingine. Mnamo Julai 26, mkuu wa diplomasia ya Ulaya na mratibu wa ripoti ya nyuklia ya Iran, Josep Borrell, aliwasilisha rasimu ya maelewano na kuzitaka pande zinazohusika katika mazungumzo hayo kukubali ili kuepusha "mgogoro hatari".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.