Pata taarifa kuu
MAREKANI- ISRAELI

Marekani na Israeli kushirikiana kuizuia Iran kutengeneza silaha ya nyukilia

Rais wa Marekani Joe Biden na waziri mkuu wa Israeli Yair Lapid wameazimia kushirikiana kuzia Iran kutengeneza silaha ya nyukilia.

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na waziri mkuu wa Israeli Yair Lapid.
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa na waziri mkuu wa Israeli Yair Lapid. © AP Photo/Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili wametia saini maazimio hayo baada ya kufanya kikao cha pamoja magharibi wa Jerusalem katika siku ya pili ya zaira ya rais Joe Biden katika mataifa ya mashariki ya kati.

Biden aidha amefanya kikao kupitia njia ya video na viongozi wa India na wale wa mataifa ya falme za kiarabu.

Makubaliano ya mataifa hayo mawili yanaeleza kuwa Marekani itatumia uwezo wake kudhibiti uwezo wa Iran wa kujihami na silaha ya nyukilia.

Marekani vile vile ikariri msimamo wake wa kuendelea kutoa msaada wa kijeshi kwa Israeli.

Iran imekuwa ikisisitiza kuwa mpango wake wa kujenga kinu cha nyukilia hautakuwa na madhara yoyote na haina nia ya kujenga bomu la nyukilia.

Biden aliwasili nchini Israeli jumatano ya wiki hii ikiwa zaira yake ya kwanza tangu achukuwe madaraka 2021.

Siku ya Ijuma Biden anatarajiwa kukutana na rais wa mamlaka ya palestina Mahmoud Abbas mjini Bethlehem wakati ambapo atazuru eneo la ukingo wa magharibi.

Maandamano yanatarajiwa kushuhudiwa mjini Bethlehem na Ramallah, ikitajwa kuwa njia moja ya kupinga ziara ya Biden na sera za Marekani kwa Palestina.

Uhusiano wa Marekani na Palestina umeonekana kudorora zaidi kufuatia mauwaji ya hivi punde ya mwanahabari wa Al Jazeera Shireen Abu Akleh Mei 11.

Mwanahabari huyo alipigwa risasi na wanajeshi wa Israeli wakati akiripoti kuhusu uvamizi wa wanajeshi wake kwenye eneo la Jenin katika ukingo wa magharibi.

Licha ya ripoti ya umoja wa mataifa kusema kuwa mwanahabari huyo aliuawa na wanajeshi wa Israeli, Marekani nayo inasema hakuna ushaidi unaonyesha risasi ilifyatuliwa kimakusudi.

Familia yake imetuma barua rasimi kutaka kukutana na Biden wakati wa ziara yake.

Siku ya jumatano Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken alizungumza na familia ya Abu Akleh kwa njia simu ambapo amewaalika kwa mkutano jijini Washington.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.