Pata taarifa kuu
URUSI- USALAMA

Putin kuzuru Iran kujadili upatikanaji wa "amani" nchini Syria.

Wakati huu ambapo mapigano yakiendelea kushika kasi nchini Ukraine, rais wa Urusi Vladimir Putin, wiki ijayo anatarajiwa kusafiri kuelekea Iran kuhudhuria kongamano kuhusu Syria ambapo atakutana na mwenzake wa Iran Ebrahim Raisi na Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki.

Vladimir Putin- Rais wa Urusi.
Vladimir Putin- Rais wa Urusi. AP - Yury Kochetkov
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya Msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov inaeleza kuwa safari ya rais kuelekea Tehran imepangwa kufanyika Julai 19 ambapo viongozi hao pia wanatarajiwa kujadili kuhusu upatikanaji wa amani nchini Syria.

Urusi, Uturuki na Iran kwa miaka kadhaa sasa zimekuwa zikifanya mazungumzo yaliopewa jina la “Astana peace process” kama njia moja ya kumaliza machafuko ya zaidi ya miaka 11 katika taifa hilo la mashariki ya kati.

Mataifa ya Urusi na  Iran yamekuwa yakitoa msaada wa kijeshi kwa Syria pamoja na kumunga mkono rais Bashar al-Assad,wakati Uturuki nayo iktoa mchango wake wa kijeshi kwa wanajeshi wa Syria na makundi mengine ya waasi yanayopigana dhidi ya vikosi vya al-Assad kaskazini mashariki mwa taifa hilo.

Hii ni zaira ya pili kwa rais Putin nje ya nchi tangu awatume wanajeshi wake nchini Ukraine mwezi Feburuari, alifanya zaira nyengine nchi ya Urusi nchini Tajikistan mwishoni mwa mwezi Juni.

Urusi na Iran ni washirika wa karibu, Uturuki nayo ikionekana kuwa mpatanishi wakati wa mapigano ya nchini Ukraine.

Tanagazo la Urusi kuwa itazuru Iran limekuja  siku moja baada ya ripoti ya Marekani kusema kuwa Moscow inaomba msaada wa ndege za kivita zisizo na rubani kutoka kwa Iran kwa minajili ya kupiga jeki jeshi lake lililoko nchini Ukraine.

Haya yanajiri wakati huu msururu mpya mazungumzo kati ya Urusi, Ukraine, Uturuki na umoja wa mataifa kuhusu uwagizaji wa nafaka kutoka Ukraine yanapotarajiwa kufanyika siku ya jumatano jijini Istanbul kimeripoti kituo cha habari cha Interfax kikimunuku waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.