Pata taarifa kuu

Nyuklia ya Iran: Mazungumzo yaanza tena Vienna baada ya kusimama kwa miezi 5

Hii ni mara ya kwanza tangu mwezi wa Machi. Wapatanishi wote katika mpango wa nyuklia ya Iran wamekutana Alhamisi hii, Agosti 4 huko Vienna, Austria. Baada ya mazungumzo kusimama kwa miezi kadhaa, watajaribu kufufua makubaliano ya mwaka 2015 ambayo yanalenga kuzuia Iran kupata silaha za atomiki.

Mwanadiplomasia wa Irani Ali Bagheri Kani, anayesimamia mazungumzo ya nyuklia, katika Ikulu ya Coburg huko Vienna, Agosti 4, 2022.
Mwanadiplomasia wa Irani Ali Bagheri Kani, anayesimamia mazungumzo ya nyuklia, katika Ikulu ya Coburg huko Vienna, Agosti 4, 2022. AFP - ALEX HALADA
Matangazo ya kibiashara

Wapatanishi kutoka Urusi, China na Iran wamekuwa wakipishana katika Ikulu ya Cobourg huko Vienna siku ya Alhamisi. Walipokelewa na mratibu wa Umoja wa Ulaya, Enrique Mora, anayesimamia mazungumzo hayo.

Baada ya kushindwa kwa mazungumzo ya mwisho nchini Qatar mwishoni mwa mwezi Juni, kati ya Iran na Marekani, Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell aliwasilisha rasimu ya maelewano Julai 26 na kuzitaka pande husika kuepuka "mgogoro hatari". Tehran na Washington zote zina nia ya kuweka mkondo wa kidiplomasia hai kwa kukosa chaguzi bora, wataalam wanabainisha.

Iran pia iliweka mawazo mezani, wakati Marekani, ambayo inashiriki katika mazungumzo haya mapya huko Vienna kwa njia isiyo ya moja kwa moja, inasalia kuwa makini kuhusu matokeo yakeo. "Matarajio yetu yapo lakini Marekani (...) iko tayari kwa nia njema kujaribu kupata makubaliano", aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter mjumbe huyo wa Washington.

Lengo ni kufufua mkataba wa 2015 unaopaswa kuzuia Iran kupata silaha za atomiki. Baada ya Marekani kujiondoa kwa upande mmoja katika makubaliano hayo mwaka 2018, na kurejeshwa kwa vikwazo dhidi ya Tehran, Iran ilianza tena shughuli zao za nyuklia kwa nguvu mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.