Pata taarifa kuu
IRAN-NYUKLIA

Nyuklia: Iran yaona ishara za Marekani hazitoshi kuondoa vikwazo

Serikali ya Marekani imetoa msamaha ambao utawezesha baadhi ya nchi kama vile Urusi, China au nchi za Ulaya kushirikiana na Iran katika miradi ya nyuklia ya kiraia, hasa kuhusiana na kituo cha Bouchehr, kinu cha maji mazito cha 'Arak au kinu cha utafiti cha Tehran. Lakini uamuzi wa Marekani ulipokelewa kwa shingo upande na Tehran.

Kituo cha kurutubisha madini ya urani cha Bushhr kusini mwa Iran.
Kituo cha kurutubisha madini ya urani cha Bushhr kusini mwa Iran. © Majid Asgaripour/Mehr News Agency/REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Marekani hautoshi, amesema msemaji wa wizara ya Mambo ya Nje wa Iran. Ishara ya Washington haitakuwa na athari za kiuchumi, ni mchezo tu kwa upande wa Marekani, imeongeza tovuti ya habari iliyo karibu na Baraza Kuu la Usalama.

Vikwazo vya Marekani kwa hakika vimeathiri sana uchumi wa Iran, hasa kwa kupunguza kwa kiasi kikubwa mauzo ya mafuta ya Tehran na mahusiano ya benki na dunia nzima.

Ali Shamkhani, mkuu wa Baraza hilo linalosimamia mazungumzo ya nyuklia, kwa upande wake alithibitisha kwamba hakuna makubaliano yanayoweza "kuweka kikomo haki ya Iran ya kuendeleza shughuli zake za utafiti na maendeleo na kuhifadhi uwezo na mafanikio ya nchi."

Shinikizo

Ni njia kwa Tehran kuimarisha sauti yake kwani mazungumzo huko Vienna yanatarajiwa kuanza tena katika siku zijazo. Tehran inataka kuondolewa kwa vikwazo vyote vilivyowekwa tangu mwaka 2018 na Marekani, masharti ambayo Washington hatajondoa kwenye makubaliano mapya ya nyuklia kabla ya kusitisha tena mpango wake wa atomiki.

Hata hivyo Marekani imesema wazi kuwa haiwezi kuondoa vikwazo hivyo vyote na kutoa hakikisho kuwa rais mwengine wa Marekani hataiondoa tena Marekani kwenye makubaliano ya nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.