Pata taarifa kuu

Nyuklia ya Iran: Mazungumzo yaanza tena, Tehran yataka vikwazo viondolewe

Siku kumi baada ya duru ya saba ya mazungumzo kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran, mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Tehran na Washington yalianza tena Jumatatu wiki hii.

Coburg, ambapo mazungumzo ya nyuklia ya Iran yanafanyika, huko Vienna, Austria, Desemba 17, 2021.
Coburg, ambapo mazungumzo ya nyuklia ya Iran yanafanyika, huko Vienna, Austria, Desemba 17, 2021. © VLADIMIR SIMICEK / AFP
Matangazo ya kibiashara

Iran inataka kuondolewa kwa vikwazo vya Marekani kabla ya uamuzi wowote kuchukuliwa, wakati nchi za Magharibi, wamebani kwamba mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia na kuondolewa kwa vikwazo lazima viende sambamba.

Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja kati ya Iran na Marekani katika kujaribu kuokoa makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015 yalianza tena Jumatatu, Desemba 27, Tehran itaka vikwazo vya Marekani viondolewe dhidi yake.

Mazungumzo ya awamu ya saba, ya kwanza tangu uchaguzi wa mwezi Juni mwaka jana wa rais wa Iran Ebrahim Raïssi mwenye msimamo mkali, yalimalizika siku kumi zilizopita baada ya Iran kudai mabadiliko makubwa katika rasimu ya makubaliano yaliyopo.

"Ikiwa tutafanya kazi kwa bidii katika siku na wiki zijazo, tunapaswa kupata matokeo mazuri. Itakuwa ngumu, maamuzi magumu ya kisiasa yatalazimika kuchukuliwa, kwa upande wa Tehran na Washington," mjumbe wa Umoja wa Ulaya, Enrique Mora amesema.

Enrique Mora alikuwa akizungumza mara baada ya kuanza tena kwa mazungumzo, ambapo wawakilishi wa Ujerumani, China, Ufaransa, Uingereza, Iran na Urusi wanashiriki, kwa uratibu wa Umoja wa Ulaya.

"Kuna hali ya udharura kati ya wajumbe wote waliopo ili mazungumzo yote yakamilike ndani ya muda muafaka. Sitatoa tarehe maalum, lakini tunazungumza wiki na sio miezi," amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.