Nyuklia: Tehran na Washington kufanya mazungumzo juu ya kuondolewa kwa vikwazo
Iran na Marekani zitaanza mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja "wiki hii" ambayo yatalenga "kuondoa vikwazo" vilivyowekwa na Washington. Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imetangaza.
Imechapishwa:
"Nchi ya Ghuba ya Uajemi itakuwa mwenyeji wa mazungumzo na mkutano kati ya Iran na Marekani utakaofanyika wiki," msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Saeed Khatibzadeh amesema wakati wa mkutano wa kila wiki.
Kauli hii inafuatia tangazo la Jumamosi la Umoja wa Ulaya na Iran la kuanza tena "katika siku zijazo" mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Iran - mazungumzo ambayo yaliyositishwa kwa zaidi ya miezi mitatu - Hayo yalibainishwa na mkuu wa diplomasia wa EU, Josep Borrell wakati wa ziara ya kushtukiza huko Tehran.
Ili kuendeleza mchakato huo, Josep Borrell alionyesha kwamba mazungumzo "yasiyo ya moja kwa moja" kati ya Marekani na Iran yatafanyika haraka "katika nchi ya Ghuba".
"Tunachoenda kufanya katika siku zijazo hakihusu mwelekeo wa nyuklia, lakini tofauti zilizopo katika suala la kuondolewa kwa vikwazo," amesema Khatibzadeh.