Pata taarifa kuu

Iran: Watengenezaji wa ndege zisizo na rubani wakabiliwa na vikwazo vya Marekani

Marekani yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Iran na hasa dhidi ya sekta yake ya uzalishaji wa ndege zisizo na rubani. Vifaa ambavyo Tehran imeanza kuiuzia Urusi kwa ajili ya vita vyake nchini Ukraine. 

Katika wiki za hivi karibuni, vyanzo vya Magharibi vimeripoti ununuzi wa Urusi wa silaha za Iran na Korea Kaskazini, zikiwemo ndege zisizo na rubani za "Shahed" na "Mohajer" za Iran. Hapa kwenye picha, hii ni ndege isiyo na rubani aina ya "Shahed".
Katika wiki za hivi karibuni, vyanzo vya Magharibi vimeripoti ununuzi wa Urusi wa silaha za Iran na Korea Kaskazini, zikiwemo ndege zisizo na rubani za "Shahed" na "Mohajer" za Iran. Hapa kwenye picha, hii ni ndege isiyo na rubani aina ya "Shahed". AFP - HO
Matangazo ya kibiashara

Hii inaitwa kuua ndege wawili kwa jiwe moja: kwa vikwazo hivi vipya, Washington inafanya kazi dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na dhidi ya Walinzi wa Mapinduzi ya Iran. Katika wiki za hivi karibuni, vyanzo vya Magharibi vimeripoti ununuzi wa Urusi wa silaha za Iran na Korea Kaskazini, zikiwemo ndege zisizo na rubani za Shahed za Iran na Mohajer.

Makampuni kadhaa yalengwa

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa Wizara ya Fedha ya Marekani, makampuni kadhaa ya Iran yanayozalisha ndege hizi zisizo na rubani au vifaa vyake pamoja na shirika la usafiri zinalengwa. Mmoja wa viongozi wa kampuni hizi pia analengwa na vikwazo vy Marekani.

Kwa kuzuia mali na ndege za mashirika hayo na watu, Marekani inataka kuzuia usambazaji wa ndege zisizo na rubani za Iran kwa Urusi. Na bado kwa mujibu wa Washington, kampuni hii ya kutengeneza ndege zisizo na rubani za Iran pia huhudumia Walinzi wa Mapinduzi, jeshi la kiitikadi la Tehran, lililojumuishwa kwenye orodha ya Marekani ya mashirika ya kigaidi.

Iran inatuhumiwa kuwapa silaha washirika wake

Kupitia Walinzi wa Mapinduzi, Iran inashutumiwa mara kwa mara kwa kuwapa silaha washirika wake wa kikanda huko Lebanon, Iraq au Yemen, ikiwa ni pamoja na kuwapa ndege zisizo na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.