Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Ndege yaondoka Sanaa kuelekea Saudi Arabia, kwa mara ya kwanza tangu 2016

Ndege ya kibiashara kutoka mji mkuu wa Yemen unaodhibitiwa na Wahuthi imefanya safari yake kwenda nchini Saudi Arabia kwa mara ya kwanza tangu 2016 Jumamosi (Juni 17), ikiwa na mahujaji kwa ajili ya Hija, ishara ya hivi karibuni ya kupunguza hali ya wasiwasi baada ya miaka kadhaa ya vita.

Wafungwa wa Huthi wanawasili katika uwanja wa ndege wa Sanaa, Ijumaa, Aprili 14, 2023. Mabadilishano ya wafungwa zaidi ya 800 wanaohusishwa na vita vya muda mrefu vya Yemen yalianza Ijumaa, shirika la kiimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu ilisema. Operesheni hizo za siku tatu zilishuhudia ndege zikisafirisha wafungwa kati ya Saudi Arabia na mji mkuu wa Yemen, Sanaa, unaoshikiliwa kwa muda mrefu na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.
Wafungwa wa Huthi wanawasili katika uwanja wa ndege wa Sanaa, Ijumaa, Aprili 14, 2023. Mabadilishano ya wafungwa zaidi ya 800 wanaohusishwa na vita vya muda mrefu vya Yemen yalianza Ijumaa, shirika la kiimataifa la Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu ilisema. Operesheni hizo za siku tatu zilishuhudia ndege zikisafirisha wafungwa kati ya Saudi Arabia na mji mkuu wa Yemen, Sanaa, unaoshikiliwa kwa muda mrefu na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran. AP - Hani Mohammed
Matangazo ya kibiashara

Ndege ya shirika la ndege la Yemenia Airways iliyokuwa na abiria 277 iliondoka mwendo wa saa mbili usiku saa za Yemen (sawa na saa moja usiku saa za Afrika ya Kati), afisa mmoja ameliambia shirika la habari la AFP, miaka saba baada ya kuzingirwa kwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sanaa na muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ambao unapambana na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran.

Ndege hiyo ni ya kwanza tangu muungano wa kijeshi ufunge uwanja wa ndege wa Sanaa mnamo mwezi Agosti 2016, zaidi ya mwaka mmoja baada ya kuanza kwa kampeni ya kijeshi ya Saudi Arabia ya kuwaangamiza Wahouthi. Mamia ya maelfu ya watu wameuawa katika mapigano hayo au kutokana na sababu zisizo za moja kwa moja kama vile ukosefu wa chakula au maji katika kile ambacho Umoja wa Mataifa unakiita mojawapo ya majanga makubwa zaidi ya kibinadamu duniani.

Lakini licha ya mashambulizi ya anga ya muungano na mapigano ya ardhini, Wahuthi, ambao walichukua udhibiti wa mji wa Sanaa mnamo mwaka 2014 na kuiondoa serikali inayotambuliwa kimataifa, wanatawala maeneo makubwa ya nchi. Moja ya nguzo tano za Uislamu, Hija ambayo itafanyika mwaka huu mwishoni mwa mwezi Juni, ina mfululizo wa ibada zinazotakiwa kutekelezwa kwa muda wa siku tano, huko Makka na maeneo jirani, na Muislamu yeyote ambaye ana uwezo, angalau mara moja katika maisha yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.