Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

Vita nchini Yemen: Serikali na waasi wabadilishana tena wafungwa

Operesheni kubwa ya kubadilishana wafungwa imeanza Ijumaa, Aprili 14 nchini Yemen kati ya kambi hasimu, limetangaza shirikisho la Kimataifa la Msalaba na Ilani Nyekundu (ICRC), ambayo inasimamia operesheni hiyo. Hatua hiyo inakuja wakati Saudi Arabia, ambayo inaunga mkono serikali, inataka kufanya mazungumzo na waasi katika nchi hii iliyoharibiwa na vita tangu 2014.

Wafungwa walioachiliwa huru wanakutana tena na familia zao katika uwanja wa ndege wa Sanaa mnamo Aprili 14, 2023. Serikali ya Yemen na waasi wamekubali kubadilishana wafungwa kwa siku tatu.
Wafungwa walioachiliwa huru wanakutana tena na familia zao katika uwanja wa ndege wa Sanaa mnamo Aprili 14, 2023. Serikali ya Yemen na waasi wamekubali kubadilishana wafungwa kwa siku tatu. REUTERS - KHALED ABDULLAH
Matangazo ya kibiashara

Ni miaka miwili na nusu sasa tangu operesheni hiyo ya kubadilishana wafungwa kati ya serikali ya Yemen na waasi ifanyike. Mara ya mwisho ilikuwa mwezi Oktoba 2020, wakati wafungwa zaidi ya 1,000 waliachiliwa kwa saa 48.

"Ndege ya kwanza iliondoka Sanaa" kama sehemu ya mabadilishano yaliyoanza siku ya Ijumaa, amesema Jessica Moussan, afisa wa uhusiano na vyombo vya habari katika ICRC. Ndege hiyo iliyotokea katika mji mkuu unaodhibitiwa na waasi wa Houthi, kuelekea Aden, mji wa bandari ulioko chini ya kilomita 400 kusini, ambako serikali inayoungwa mkono na Saudi Arabia ina makao yake kwa muda.

Mwishoni mwa mwezi Machi, serikali ya Yemen inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa na waasi wakiungwa mkono na Iran walifikia makubaliano mjini Bern, Uswisi kubadilishana wafungwa zaidi ya 880 wakiwemo Wasaudi na Wasudan. Mchakato wa kubadilishana wafungwa utafanyika kwa siku tatu katika maeneo mbalimbali ya Yemen na Saudi Arabia, ICRC imesema katika taarifa yake.

"Kwa ishara hii ya nia njema, mamia ya familia zilizosambaratishwa na migogoro zitaunganishwa tena kwa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtkufu wa Ramadhani, na kuleta mwanga wa matumaini katikati mwa mateso makubwa," amesema Fabrizio Carboni, mkurugenzi wa ICRC katika Mashariki ya Kati. Anatumai kwamba "matoleo haya yanatoa msukumo kwa suluhisho pana la kisiasa".

Matumaini ya mapatano mapya

Kufufuliwa kwa uhusiano kati ya Saudi Arabia na Iran mwanzoni mwa majira ya baridi kuliibua matumaini ya kusitisha mapigano nchini Yemen. Ujumbe wa Saudi ulikuwa mjini Sanaa wiki hii; uliondoka Alhamisi kukiwa na "makubaliano ya awali" tu ya kusitisha mapigano na ahadi ya "mazungumzo mapya", kulingana na afisa wa waasi.

Mazungumzo hayo yanalenga katika mapatano ya miezi sita yakifungua njia kwa kipindi cha miezi mitatu ya mazungumzo juu ya mpito ambayo yatadumu kwa miaka miwili, kulingana na vyanzo vya serikali. Ni katika kipindi hiki cha miaka miwili ambapo suluhu ya mwisho lazima lijadiliwe kati ya pande zote.

Makubaliano hayo yanapaswa kufanya iwezekanavyo kukidhi matakwa mawili makuu ya waasi wa Houthi: malipo ya serikali ya mishahara ya watumishi wa umma katika maeneo ya waasi na kufunguliwa tena kwa uwanja wa ndege wa Sanaa, unaodhibitiwa vikali na kikosi cha wanaanga cha Saudia.

Mnamo 2022, kati ya mwezi Aprili na Oktoba, wahusika walikuwa tayari wamezingatia makubaliano ya miezi sita. Ingawa haikusasishwa rasmi baada ya kumalizika muda wake katika msimu wa joto, hali iliendelea kuwa shwari chini.

Tangu kuanza kwa mzozo huo, miaka minane iliyopita, kisha uingiliaji wa kijeshi wa Saudi Arabia mnamo 2015, Yemen imekuwa ikipitia moja ya machafuko mabaya zaidi ya kibinadamu ulimwenguni. Idadi ya waliofariki ni mamia ya maelfu na waliokimbia makazi ni mamilioni. Njaa na magonjwa vimeathiri raia; robo tatu ya Wayemeni sasa wanategemea misaada ya kimataifa. Msaada unaoendelea kupungua.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.