Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

UN: Pande zinazokinzana zafikia makubaliano ya usitishwaji vita kwa miezi miwili Yemen

Umoja wa Mataifa umetangaza Ijumaa Aprili 1 kwamba pande zinazokinzana nchini Yemen zimefikia makubaliano ya usitishwaji mapigano kwa kipindi cha miezi miwili. Makubaliano hayo yataanza kutekelezwa Jumamosi Aprili 2 saa moja usiku.

Mwanajeshi wa Yemen, inayoungwa mkono na muungano unaoongoza na Saudi Aarabia, akifyatua risasi wakati wa mapigano na waasi wa Houthi karibu na mji wa Marib mnamo Juni 20, 2021.
Mwanajeshi wa Yemen, inayoungwa mkono na muungano unaoongoza na Saudi Aarabia, akifyatua risasi wakati wa mapigano na waasi wa Houthi karibu na mji wa Marib mnamo Juni 20, 2021. AP - Nariman El-Mofty
Matangazo ya kibiashara

Pande zinazopigana katika vita nchini Yemen, ambavyo vinawakabili waasi wa Houthi dhidi ya vikosi vinavyounga mkono serikali vinavyoungwa mkono na muungano wa kimataifa unaoongozwa na Saudi Arabia, vimekubali kufikiwa kwa makubaliano ya miezi miwili. Makubaliano hayo yanaanza kutekelezwa Jumamosi hii, kukiwa na uwezekano wa kurefusha kipindi hiki, Umoja wa Mataifa umetangaza Ijumaa.

"Wapiganaji wameitikia vyema pendekezo la Umoja wa Mataifa la kusitishwa mapigano kwa kipindi cha miezi miwili ambacho kitaanza kutekelezwa kesho saa moja usiku jioni," mjumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Yemen Hans Grundberg amesema katika taarifa.

Taarifa zaidi zinakuja

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.