Pata taarifa kuu

Saudi Arabia yajibu mashambulizi ya Houthi dhidi ya vituo vyake vya mafuta

Nchini Yemen, miaka saba baada ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia, kuanza kuingilia kati kijeshi, muungano huo unasema kuwa umefanya mashambulizi ya anga kwenye bandari ya Hodeidah na katika mji mkuu wa Sanaa.

Wapiganaji wa Houthi wakitathmini uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya anga ya usiku ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya mji mkuu wa Sanaa unaoshikiliwa na waasi wa Houthi mnamo Machi 26, 2022.
Wapiganaji wa Houthi wakitathmini uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya anga ya usiku ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya mji mkuu wa Sanaa unaoshikiliwa na waasi wa Houthi mnamo Machi 26, 2022. AFP - MOHAMMED HUWAIS
Matangazo ya kibiashara

Mashambulizi haya ya anga yamefanyika ili kujibu mashambulizi ya waasi wa Houthi siku ya Ijumaa dhidi ya mitambo ya mafuta ya Saudi Arabia. Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unahakikisha kwamba umejibu "kulinda vyanzo vya nishati duniani".

Katikati msukosuko wa nishati duniani unaohusishwa na vita vya Ukraine na vikwazo dhidi ya Urusi, Saudi Arabia, nchi inayoongoza kwa uzalishaji wa mafuta ghafi duniani, inasisitiza bila hofu kuwa lengo la mashambulizi haya ni "kuhakikisha utendakazi wa mitambo ya usambazaji wa nishati.

Mashambulio ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yamelenga miundombinu ya mafuta na umeme katika bandari ya Hodeidah, kulingana na kituo cha televisheni ya Yemen inayodhibitiwa na waasi wa Houthi. Mjini Sanaa, jengo la utawala la kampuni ya mafuta pia limelenwa na mashambulizi hayo anga, kulingana na shuhuda zilizokusanywa na shirika la habari la Reuters.

Muungano wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia na kuungwa mkono hasa na Umoja wa Falme za Kiarabu umehakikisha kwamba huo ulikuwa mwanzo tu wa majibu yake, na kwamba Wahouthi, ambao wanaungwa mkono na Iran, lazima "wafikirie athari ya tabia yao ya uhasama.

Ijumaa, Machi 25, mashambulizi ya waasi wa Houthi yalisababisha mlipuko wa matangi mawili ya kampuni kubwa ya mafuta ya Aramco, huko Jeddah. Moto huo ulionekana kwenye njia ya mzunguko wa mashindano ya Formula 1 ambapo mashindano ya Saudi Arabian Grand Prix yatafanyika Jumapili hii. Mashindano ambayo ytafanyika, kama ilivyopangwa, kulingana na waandaaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.