Pata taarifa kuu
YEMEN-USALAMA

Yemen: Watu kadhaa wauawa katika shambulizi la muungano

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia umetekelesha shambulizi la anga mji wa Hodeidah, mji ulioko magharibi mwa Yemen unaodhibitiwa na waasi wa Houthi, usiku wa Alhamisi Januari 20 kuamkia Ijumaa Januari 21, na kuharibu kituo cha mawasiliano na kusababisha kukatika kwa intaneti nchini kote, shirika lisilo la kiserikali limesema Ijumaa.

Picha ya video iliyopigwa na Kituo cha vyombo vya habari vya Ansarullah mnamo Januari 21, 2022 ikionyesha uharibifu umliofanywa na shambulizi la muungano unaoongozwa na Saudi katika kituo cha mawasiliano katika mji wa bandari unaoshikiliwa na waasi wa Hodeidah nchini Yemen, shambulizi ambalo limesababisha kukatika kwa mtandao wa intaneti nchini kote.
Picha ya video iliyopigwa na Kituo cha vyombo vya habari vya Ansarullah mnamo Januari 21, 2022 ikionyesha uharibifu umliofanywa na shambulizi la muungano unaoongozwa na Saudi katika kituo cha mawasiliano katika mji wa bandari unaoshikiliwa na waasi wa Hodeidah nchini Yemen, shambulizi ambalo limesababisha kukatika kwa mtandao wa intaneti nchini kote. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Muungano unaounga mkono serikali, ambao unapambana na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran, umesema ulikuwa unalenga "kitovu cha uharamia na uhalifu uliopangwa" katika mji huo muhimu wa bandari kwa nchi hiyo iliyokumbwa na vita.

Shirika la NetBlocks, linalojishughulisha na ufuatiliaji wa mtandao duniani kote, limeripoti "kuporomoka kwa mtambo wa intaneti nchini" baada ya milipuko hiyo. Waandishi wa habari a shirika la habari la AFP huko Hodeidah na Sanaa wamethibitisha kukatika kwa intaneti.

Kwa upande wake, shirika la habari la serikali ya Saudia limesema kuwa muungano huo ulifanya "mashambulio ya anga yaliyolenga kuharibu uwezo wa wanamgambo wa Houthi huko Hodeidah".

Wahouthi wamesema kuna watu kadhaa waliouawa katika shambulizi hilo, lakini taarifa yao haikuweza kuthibitishwa mara moja. Mwandishi wa shirika la habari la AFP huko Hodeidah ameelezea shambulio kubwa.

Haya yanajiri baada ya waasi wa Houthi kuiteka nyara meli iliyokuwa na bendera ya Umoja wa Falme za Kiarabu katika Bahari Nyekundu, ambapo muungano huo ulionya kuwa ungeshambulia kwa mabomu bandari zinazodhibitiwa na waasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.